MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA MJINI ATEMBELEA WAGONJWA NA KUTOA VITABU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARY KATIKA JIMBO HILO
Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vincent Nyerere ametembelea wagonjwa katika Hospital ya Mkoa wa Mara ambapo baadhi yao walitekwa na kukatwa mapanga juzi.
Mheshimiwa Nyerere akimjulia hali mgonjwa katika hospital ya mkoa wa Mara ambaye ni mmoja ya wahanga ambao walitekwa na majambazi kisha kunyang'anywa fedha na mali zao
Mheshimiwa Nyerere akimjulia hali mgonjwa katika hospital ya mkoa wa Mara leo,mzee huyu ana umri wa miaka 67 lakini cha ajabu ameshindwa kupata huduma stahiki kwa kile kinachosemekana hana fedha lakini wadau sera ya wazee inasemeaje? kilio chake kimefika kwa mheshimiwa Nyerere
Mheshimiwa Nyerere akimjulia hali mgonjwa katika hospital ya mkoa wa Mara leo,huyu aliwahi kuwa katibu wa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini na katika maelezo yake anasema kuwa majambazi waliomvamia kwake walikuwa zaidi ya nane na walipofanikiwa kuingia walimkata panga kama uonavyo picha hiyo na kisha kuchukua redio na fedha kiasi cha laki nane lakini baadaye redio zilipatikana maeneo ya uwanja wa ndege
Hivi ni vitabu ambavyo vilitolewa na mheshimiwa mbunge wa jimbo Musoma mjini Vincent Nyerere katika kusaidia sekta ya elimu ndani ya jimbo la Musoma mjini
Waswahili nanasema elimu ndio msingi wa maisha ya mtanzania na ndio itakuwa dira nzuri katika kuondoa umaskini jimboni Musoma
Walimu wa shule mbalimbali katika jimbo la Musoma mjini wakiangalia vitabu ambavyo vimeletwa na mbunge wa jimbo hilo
Baada ya kuwa katika viwanja vya Manispaa ya Musoma mara akatokea Afisa Utamaduni katika manispaa hiyo Shekdad na kuanza kulonga juu ya vitabu hivyo na suala zima la michezo
Maelezo bado yanaendelea kati ya afisa utamaduni na Mheshimiwa Nyerere
Mashuhuda katika ugawaji wa vitabu hivyo walikuwepo kama wanavyoonekana Mwarabu kushoto ambaye ni mpiga picha wa ITV na mtangazaji kutoka Victoria fm ya mjini Musoma
Elimu Kwanza
Mwana wa Afrika pia alipata nafasi ya kubadilishana mawazo na Afisa utamaduni wa Manispaa kuhusu masuala ya kimichezo katika manispaa hiyo,mbali na hapo alikuwa akipongeza kauli ya mbunge juu ya dhamira yake ya kuendeleza michezo
PICHA NA HABARI NI KUTOKA KWA www.mwanawafrika.blogspot.com
PICHA NA HABARI NI KUTOKA KWA www.mwanawafrika.blogspot.com
Comments
Post a Comment