Askari JWTZ ahukumiwa miaka 30 jela kwa kunajisi


Mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Mbalizi, Saje Michael (44) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 na kulipa faini ya Sh1milioni baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi mtoto wa mtalaka wake. Mtoto aliyenajisiwa anadaiwa kuwa na umri wa miaka mitatu.

Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo. Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Maria Amosy baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka.Ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wakili wa Serikali Christina Joasy kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 5, mwaka jana, nyumbani kwake Mbalizi Mtaa wa Mtakuja katika Halmashauri ya Mbeya.

Upande wa mashtaka ulidai mshtakiwa alimdhalilisha mtoto huyo nyumbani kwake walipopitia nyumbani kwake wakati wakielekea kwa bibi yao mzaa mama ambaye anaishi Mbalizi mkoani hapa.Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka mtalaka wake walipoachana na mume huyo alienda kuolewa na mume mwingine ambaye ndiye mwenye mtoto ambaye alifanyiwa unyama huo.

Alisema mtoto alipelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kukutwa ameambukizwa magonjwa ya zinaa.Mwendesha mashtaka alimwomba hakimu kutoa adhabu kali ili liwe fundisho kwa watu wenye tabia kama mshtakiwa.

Wakati huohuo mkazi wa Uyole jijini hapa Hussein Msuya (18) alifikishwa mahakamani hapo kwa shtaka la kubaka watoto wawili wa familia moja wenye umri wa miaka saba (majina yanahifadhiwa).Akisomewa shtaka hilo na wakili wa Serikali Griffin Mwakapeje alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 25, mwaka huu katika maeneo ya Uyole sokoni.

Mshtakiwa alikana kosa hilo na Hakimu Mkazi, Venance Mlingi aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 30, mwaka huu. Mshtakiwa alirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

- via Mwananchi

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA