NDEGE 8 ZATUA DAR KWA AJILI YA ZIARA YA RAIS OBAMA
DAR ES SALAAM. MAKACHERO wa Marekani wameendelea na matayarisho ya mwisho ya ziara ya Rais Barack Obama, ambapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walikuwa na kazi ya kuunganisha helikopta za doria. Makachero hao walikuwa wakiunganisha helikopta sita zilizosafirishwa vipande vipande kutoka Marekani, ambapo meli mbili za kivita na ndege moja pia zimewasili. Rais Obama tayari yuko katika ardhi ya Afrika, ambapo leo anatarajiwa kwenda Afrika Kusini baada ya kumaliza ziara yake ya kwanza Senegal na anatar ajiwa kuwasili nchini Jumatatu. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa jana na Mwananchi unaonyesha Marekani imeleta helikopta hizo kwa ajili ya ulinzi wa Rais Obama, zikiwemo meli zilizobeba helikopta nyingine mbili na ndege. Habari zilizopatikana kutoka kwa wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Ki