MKUU WA MKOA WA MWANZA AFUNGUA KAMPENI YA USAFI JIJINI MWANZA
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh.Evarist Ndikiro amefungua rasmi kampeni ya kuweka jiji la Mwanza katika hali ya usafi akishirikiana kwa ukaribu kabisa na Meya wa jiji la Mwanza Mh.Stanslaus Mabula, kampeni hii imeandaliwa na Halmashauri ya jiji la Mwanza ikishirikiana kwa ukaribu kabisa na chuo kikuu cha mtakatifu Agustino (SAUT) kilichopo jijini hapa.
Kampeni hii inalengo la kutoa elimu na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuliweka jiji la Mwanza katika hali ya usafi, kampeni hii imekuwa na kauli mbiu hii
"Pamoja Tuliweke Jiji letu safi"
Mkuu wa mkoa wa mwanza MH.Evarist Ndikiro akiwa na baadhi ya viongozi wengine wa jiji la Mwanza katika kuzindua kampeni ya usafi leo katika jiji la mwanza. |
Wa pili kutoka kushoto ni meya wa jiji la mwanza na kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa mwanza Mh.Ndikiro wakifanya usafi |
Mkuu wa mkoa wa mwanza akipewa mfagio |
Mkuu wa mkoa wa Mwanza akishika mfangio kama ishara ya kushirikiana na wakazi wa jiji la mwanza katika suala nzima la usafi. |
Baadhi ya wanachama wa SSPRA kutoka chuo cha SAUT wakishiriki katika kufanya usafi pia. |
hawa ni baadhi wa wakazi wa jiji la mwanza wakiwa katika zoezi la usafi ililofunguliwa leo na mkuu wa mkoa wa mwanza MH.Evarist Ndikiro Baadhi ya wanachama wa sspra wakifanya usafi. Kutoka kushoto ni rasi wa chuo cha mtakatifu augustino Mh. Dovakmwene Mscheshi akifanya usafi pamoja na wakazi wa jiji la mwanza. Wakazi wa jiji la mwanza wakifany usafi Wakazi wa jiji la mwanza wakifanya zoezi la usafi leo
|
Comments
Post a Comment