UCHAMBUZI WA GEORGE MARATU JUU YA WABUNGE WA MKOA WA MARA WENYE NAFASI YA KURUDI BUNGENI, AMTAJA MBUNGE MMOJA TU MWENYE NAFASI

Utafiti huu umefanywa na mwandishi wa ITV bwana George Maratu juu wa wabunge wa mkoa wa Mara wenye nafasi ya kuweza kurudi bungeni mwaka 2015, utafiti huu nime ucopy kwa jinsi ulivyo bila ku edit chochote kutoka katika account yake ya facebook. Nikachukulia kigezo cha prominance kwa kuwa wabunge hawa wanawakilisha maeneo ambayo mimi Nyanja ninatokea.

TAHADHALI…CHANGIA HOJA HII KWA HOJA BILA KUJALI KUWA WANAOTAJWA WAKIPOTEZA UBUNGE BASI NA KITUMBUA CHAKO KITAJAA MCHANGA…Utafiti wa miezi sita iliyopita, umeonyesha wazi kwa mkoa wa Mara ni Mbunge mmoja tu anaweza kurudi 2015 kwa asilimia 80 hadi sasa…
Jimbo la Tarime mbunge Nyambari Nyangwine (CCM) kurudi kwake ni asilimia 7 tu hadi sasa,sababu hajatekeleza ahadi zake,kushindwa kutembelea wapiga kura, mbali na kuonekana wakati wa matukio tena pengine kwa kujificha jificha na kikubwa kutuhumiwa kuwa mmoja ya watu wanaongoza makundi ndani ya chama chake ingawa pia serikali yake ya CCM imesaidia kutatua baadhi ya changamoto kwa wananchi kiduchu.


Jimbo la Musoma mjini mbunge Vicent Nyerere (Chadema) kurudi kwake ni asilimia 5 ingawa chama chake bado kinakubalika,sababu kubwa kwake kushindwa kutekeleza ahadi zake mpya za mwaka 2010 alizotoa kama kuhakikisha kiwanda cha Mutex kinafanya kazi na vijana kupata ajira,kuanzisha viwanda vya kusindika mazao(Juice),kutumia konokono za pembeni ya ziwani kutengeneza chakula cha kuku,wahudumu wa bar kupata vyeti vya ualimu na kuingizwa polisi na magereza,wafungwa kutumia taaluma zao kutumikia jamii,bwawa la Kitaji kiwa sehemu ya maeneo ya Utalii,baadhi ya barabara kuwekwa lami,makundi ndani chama chake na pia kukimbiwa na wafuasi wake waliosaidia kumuingiza madarakani ni miongoni mwa changamoto kubwa kwake.

Jimbo la Musoma vijijini mbunge Nimrod Mkono (CCM) hadi sasa ametekeleza ahadi zake kwa zaidi ya aslimia 90 lakini kurudi kwake Bungeni ni majaliwa kwani kwa mujibu wa sheria jimbo hilo litakatwa kwa vile lina halmashauri mbili kamili,kama atagombea jimbo la Nyanja(Majita) ukabila lazima utakuwa kikwazo kwake na kama akiingia jimbo la Butiama suala la Ukabila na ubaguzi wa utekelezaji wa miradi pia laweza kuwa changamoto kubwa hasa katika eneo analotoka AG tarafa ya Kiagata wanaweza kumuunga mgombea kutoka eneo hilo hivyo kuzima ndoto zake za kutetea jimbo hilo kwa kipindi cha nne.
Jimbo la Serengeti mbunge Dk Stephen Kebwe (CCM) asilimia zake za kurudi Bungeni zimeongzeka kutoka aslimia 9 miezi kadhaa iliyopita hadi kufikia 38 sababu kubwa tangu ameteliwa kuwa naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii,ametumua nafasi hiyo vema kuwatembelea wapiga kura na kuanza kutekeleza baadhi ya ahadi zake ingawa pia ukabila na kundi la mtangulizi wake Dk James Wanyancha linaweza kuwa kikwazo kwake kurejea Bungeni kutokana na kundi hilo kutumia kete ya ukabila kuhakikisha wanazima ndoto yake hiyo.
Jimbo la Bunda mbunge Steven Wassira (CCM) huyu kuna fununu anaweza kujitupa katika Urais ingawa katika ahadi ametekeleza aslimia 70 na kama akipenda kurudi katika ubunge bado nafasi yake ni kubwa hasa kwa kura za vijijini,lakini changamoto kubwa itakuwa kwa kura za vijana vijijini na mjini ambapo hapo mbunge wa viti maalum Esther Bulaya nafasi yake ni kubwa , sasa kwa wote itategemea uteuzi wa chama chao CCM.

Jimbo la Rorya mbunge Lameck Airo (CCM) huyu ametekeleza ahadi zake aslimia 90 hadi sasa katika jimbo hilo na tayari ametangaza awezi kugombea lakini akisema anagombea kurudi kwake pia kutakuwa ni tatizo kubwa ukilinganisha na changamoto kubwa za ukabila na koo za jimbo hilo.
Jimbo la Mwibara mbunge Kangi Lugola(CCM) huyu ametekeleza ahadi aslimia 67 lakini uhakika wa kurudi Bungeni ni asilimia 80 kutokana na ukaribu wake kwa wapiga kura pia kutetea maslahi ya jimbo lake na kutanguliza mbele maslahi ya taifa lake si chama chake….HUYU NDIYE MBUNGE PEKEE MWENYE TEGEMEO MKOANI MARA………

Changia hoja na kurekebisha kama utakavyoona ukizingatia huu ni utafiti wangu binafsi baada ya kutembelea majimbo hayo yote Ingawa utafiti huu waweza kubadilika kulingana na utekelezaji wa ahadi unavyoendelea……

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA