MBONGO AUAWA KWA SUMU UJERUMANI



Marehemu Robert John Mpwata (34) enzi za uhai wake.

Na Makongoro Oging’, Issa Mnally/Uwazi

MTU mmoja anayeaminika kuwa ni Mtanzania, Robert John Mpwata (34) anadaiwa kuuawa kwa kuwekewa sumu na mwili wake kukutwa chumbani kwake katika Mji wa Shorten nchini Ujerumani siku chache zilizopita.

Habari kutoka kwa baadhi ya marafiki zake waliopo huko, zinasema Robert aliyekuwa mwanamichezo aliyecheza sarakasi, karate na judo, aliwasiliana nao kwa njia ya simu mara kwa mara na walipata taarifa za kifo chake siku saba ya kufariki dunia.

Inadaiwa kabla ya kifo cha mwanamichezo huyo, alikuwa akiwasiliana vizuri na wenzake, lakini umauti wa ghafla uliomkuta na mazingira yake, unawapa hofu kuwa huenda alifariki baada ya kuwekewa sumu.
Inadaiwa kuwa Februari 8, mwaka huu ilikuwa ni siku waliyotakiwa kufanya onyesho, kitu ambacho kiiwafanya wawe na mawasiliano ya mara kwa mara.

Mwandishi wa habari hii aliwasiliana na ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani, ambako mfanyakazi mmoja aliyekataa kutajwa jina lake kwa vile siyo msemaji, alikiri kusikia taarifa hizo, lakini akasema inakuwa vigumu kwao kutoa msaada kwa vile taarifa isiyo rasmi inasema marehemu alikutwa na vielelezo vinavyomtambulisha kuwa ni mtu wa Somalia.



Robert John Mpwata akiwa na mke wake.

Naye Mwenyekiti wa umoja wa Watanzania nchini humo, Mfundo Peter Mfundo alikiri kutokea kwa kifo hicho, kwani awali marehemu aliwaaga Watanzania wenzake kuwa ataondoka kwenda nyumbani kwa mke wake.

“Mimi nilipata taarifa kutoka kwa rafiki yake wa karibu baada ya wiki mbili tangu akutwe amefariki, hakuna anayejua kilichomuua maana serikali bado haijatoa majibu. “Mpaka sasa bado tunasubiri kutatokea nini na hata kama ikitokea tupewe maiti kuisafirisha ni kazi kwani ni zaidi ya shilingi milioni 12, nimewasiliana na baba yake anasema hana nauli ya kumleta huko.

“Robert alikuja hapa katika shughuli za sanaa na alimuoa Mjerumani aliyezaa naye mtoto Daniel ambaye ana umri wa miezi minne,” alisema kiongozi huyo.Kwa mujibu wa Peter, mke wa marehemu aliwaambia kwamba angependa amzike mumewe nchini humo ili iwe rahisi kwa mtoto wake kuhani kaburi lake.


Ndugu zake marehemu Robert John Mpwata wakiwa Bongo, (mwenye shati jekundu ni baba yake).

John Mpwata (65), baba mzazi wa marehemu akiwa nyumbani kwake Manzese Kilimahewa jijini Dar, alisema taarifa za kifo hicho zimemuumiza.“Mwanangu aliondoka mwaka 2007 kutafuta maisha huko Ujerumani na kwa mara ya mwisho niliongea naye Desemba 22, mwaka jana, aliniambia atakuja nyumbani na mkewe Mzungu hivi karibuni baada ya mwanaye Daniel kuanza kutembea.

“Lakini cha kushangaza hivi karibuni nimepata taarifa ya kifo chake, sina jinsi maana nimeambiwa uwezekano wa mwili kuletwa ni mdogo na ningependa kwenda kumzika lakini sina milioni 2.5 za nauli, ninawaomba Watanzania wanisaidie nikamzike mwanangu,” alisema na kutaja namba zake za simu kuwa ni 0689 476408 au 0713 432088.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA