Mechi ya Yanga, Simba yatinga mahakamani Dares salaam


Sweetbert Lukonge,
Dar es Salaam
KILA kukicha mechi ya Simba na Yanga huwa haiishi vituko baada ya mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Musley Al Rawah, jana kupandishwa kizimbani na kusomewa shtaka moja la kushambulia na kudhuru mwili.
Al Rawah anadaiwa kutenda kosa hilo Machi 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo siku hiyo kulikuwa na mechi ya Ligi Kuu Bara iliyozikutanisha Simba na Yanga na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Anadaiwa kumshambulia kwa kumpiga mtoto wa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji na kumsababishia majereha na maumivu makali mwilini mwake na kama kusingekuwa na mechi hiyo basi kusingekuwa na kesi hiyo.
Kutokana na hali hiyo, Manji alimfungulia mashtaka kiongozi huyo na jana Jumanne amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar ambapo alisomewa shtaka hilo.Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, Gines Teshe, akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu, Frank Moshi alisema kuwa Al Rawah ameshtakiwa kwa kosa moja tu la kushambulia na kudhuru mwili, jambo ambalo ni kosa kisheria.
Alisema Machi 8, mwaka huu, Al Rawah alimshambulia kwa kumpiga Mehbub Ally Manji katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kumsababishia majeraha na maumivu, jambo ambalo ni kosa kisheria.
Hata hivyo, Al Rawah alikanusha kutenda kosa hilo na kutakiwa kulipa dhamana, jambo ambalo alilitekeleza na kuruhusiwa kuondoka mahakamani hapo mpaka Aprili 20 kesi itakaposikilizwa tena.Hata hivyo, katika kesi hiyo, Al Rawah anasimamiwa na wakili wa kujitegemea, Dr Damas Ndumbaro.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA