matokeo ya mechi ya Super Cup FC Barcelona vs Sevilla (Pichaz&Video) Zipo hapa
Usiku wa August 11 ulikuwa ni usiku ambao unazikutanisha timu mbili kutoka Hispania ambazo zote ni mabingwa, FC Barcelona ni Bingwa wa klabu Bingwa Barani Ulaya huku klabu ya Sevilla ikiwa Bingwa wa Kombe la UEFA Europa League ambalo zamani lilikuwa linaitwa UEFA ndogo.
Mchezo ambao ulivutia wengi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya magoli hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika FC Barcelona ilikuwa na jumla ya magoli 4-4 sawa Sevilla ambapo magoli ya FC Barcelona yalifungwa na Lionel Messi dakika ya 7 na 15, Rafinhadakika ya 44 na Luis Suarez dakika ya 52, huku magoli ya Sevilla yakifungwa na Banega dakika ya 3, Antonio Reyes dakika ya 57, Gameiro dakika ya 72 na Konoplyanka dakika ya 81.
Kwa mujibu wa sheria mechi ililazimika kuongezwa dakika 30 za nyongeza hivyo kufanya mechi hiyo kumalizika kwa kucheza dakika 120 nakuifanya klabu ya FC Barcelonakuibuka na ubingwa kwa goli la Pedro Rodriguez dakika 155 ya mchezo.
Nimekusogezea picha za mechi hapo chini mtu wangu
Hii ni video ya magoli mtu wangu
Comments
Post a Comment