ARSENAL 'OUT' LIGI YA MABINGWA ULAYA

Arsene Wenger na benchi lake wakiwa hawaamini kilichotokea mbali na ushindi wao wa 2-0.
KIKOSI cha Arsenal kimetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya ushindi wake wa mabao 2-0 iliyoupata ugenini dhidi ya Monaco ya Ufaransa usiku huu.Timu hiyo imeondolewa kwa bao la ugenini licha na matokeo ya jumla kuwa 3-3.
Baadhi ya wachezaji na viongozi wa Monaco wakishangilia baada ya filimbi ya mwisho.
Katika mchezo wa kwanza Arsenal ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1 ikiwa nyumbani England, hivyo Monaco wanasonga mbele kwa ushindi wa mabao mengi ugenini kuliko vijana hao wa Wenger.
Alexis Sanchez akienda chini baada ya kuzongwa na Nabil Dirar wa Monaco.
Mabao ya jana ya Arsenal yamewekwa kimiani na Olivier Giroud dakika ya 36 na la pili likifungwa na Aaron Ramsey dakika ya 79 ya mchezo.
Giroud akipeleka hatari langoni mwa Monaco.
(Picha zote kwa hisani ya Daily Mail)

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA