MAANDALIZI YA PAMBANO LA MAYWEATHER NA MANNY PACQUIAO KILA MWANADONDI KATIKA MAZOEZI MAKALI



Muamuzi atakaekaa katikati wakati wa mpambano wa kukata ubishi baina ya Floyd Mayweather dhidi ya Manny Pacquiao atalipwa dola za kimarekani 10,000 ambazo ni sawa na Paund 6,800.
Tayari muamuzi Kenny Bayless kutoka nchini Marekani ameshatajwa kuwa muamuzi wa mpambano huo ambao utapigwa mjini Las Vegas, Mai mbili mwaka huu.
Mapambano huo ambao utapigwa kwenye ukumbi wa MGM Grand, unatarajiwa kukusanya mapato karibu dola za kimarekani million 400 ambazo ni sawa na Paund million 273.
Mayweather akipima uzito kwenye mizani, na tayari ameshafanikiwa kukata uzito wa pounds tatu na nusu.
Kizuia mdomo cha Pacquiao ambacho atakitumia wakati wa mchezo wake dhidi ya Mayweather mwezi ujao (May 2) mjini Las Vegas
Pacquiao akiwa mzoezini sehemu za Griffith Park nje kidogo ya mji wa Los Angeles mwishoni mwa juma lililopita.
Pacquiao akionyesha uwezo wa kimazoezi, kati kati ya mashabiki wake.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA