TAARIFA YA ACT TANZANIA KWA UMMA
Chama cha Wazalendo (ACT - Tanzania ) Kama mnavyofahamu, Chama cha Wazalendo ACT-Tanzania kitafanya mkutano wake mkuu na uzinduzi wa chama mnamo tarehe 28 na 29 Machi 2015. Katika mkutano Mkuu chama kitapitisha katiba mpya ya chama na kufanya uchaguzi wa nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Kiongozi wa chama, Mwenyekiti wa Chama, Makamu wenyeviti, Katibu Mkuu na Manaibu makatibu wakuu. Pia chama kitachagua wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu. Katika uzinduzi wa chama tarehe 29 Machi 2015 kuanzia saa tisa alasiri, viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wamealikwa. ACT – Tanzania imemwalika Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti wa Taifa wa CUF kuzungumza kwa niaba ya vyama vya upinzani nchini kuhusu ‘ kwa nini Tanzania bado ni nchi masikini na nini cha kufanya kuondoa umasikini’. Pia viongozi wote wa vyama vya siasa nchini, mabalozi wa nchi mbalimbali na wakuu wa asasi zisizo za kiserikali wamealikwa. Uzinduzi utaonyeshwa moja kwa moja na vituo vya tel