TAHADHARI YA WIZARA KUHUSU UTAPELI WA AJIRA YA WALIMU WAPYA 2015/2016


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU MWAKA 2015/16JIHADHARI NA MATAPELI


Kumekuwepo na Tangazo la upotoshaji kuhusu Ajira ya walimu wapya kwa mwaka 2015/16 (TANGAZO No. T.022/15TMS 2015) linalodaiwa kuwa limetolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kusambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii. Taarifa zilizotolewa katika tangazo hilo siyo za kweli na Wizara haihusiki nazo.

Aidha, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inapenda kuufahamisha umma kuwa ajira ya Walimu wa ngazi ya Cheti, Stashahada, na Shahada hufanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Ajira kutoka Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Hivyo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haihusiki moja kwa moja na zoezi hilo.

Kutokana na mgawanyo wa majukumu ya Wizara mbalimbali, taarifa sahihi kuhusu ajira mpya za walimu kwa mwaka huu wa fedha zitatangazwa na Mamlaka inayohusika yaani Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI mara watakapokamilisha taratibu zinazotakiwa.

Imetolewa na:

Katibu Mkuu,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
24 Machi, 2015

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA