Vyuo Vikuu Mbeya wamtaka Prof. Mwandosya awanie Urais


Idd Mambo (katibu Itidadi na Uendezi, Chuo Kikuu TEKU) akimkaribisha mtoaji tamko hilo

Shirikisho la Vyuo Vikuu mkoani Mbeya limefaya kongomano lililohusu uchaguzi mkuu lililofanyika katika ukumbi wa Benjamini Mkapa jijini hapa na kuchukua nafasi hiyo ya kumshawishi Prof. Mark Mwandosya kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu huu.

Akisoma tamko loa wanazuoni hao mbele ya waandishi wa habari, Katibu wa shirikisho hilo Oscar Mwaihabi kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona ndani ya chama hicho hakuna kiongozi mwenye sifa ya kufanana na Prof. Mwandosya na hivyo wameona Tanzania ijayo iongozwe na kiongozi huyo.

“Sisi wanazuoni tumeona kuwa wewe Prof. Mark J. Mwandosya unafaa kabisa kupokea kijiti cha Urais kutoka kwa Jakaya Kikwete kwa kuwa unafaa na ni tofauti na wengine wote waliojitokeza kutangaza nia katika Chama Cha mapinduzi kutokana na uongozi uliowahi kushiriki. Hujawahi kupata tuhuma yoyote mpaka leo hii, pia Taifa linahitaji kiongozi mwenye hekima na maamuzi magumu hata utafiti unaonesha uwezo ulionao wa kiuongozi,” 
amesema Mwaihabi.

Hadi sasa, wanachama waliojitokeza kuwania kuteuliwa na CCM kugombea urais ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, January Makamba (Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia), Hamisi Kigwangala, na Lazaro Nyalandu ambaye ni Waziri wa Maliasili na Utalii.

Pia wako wanaotajwa kuwania urais lakini hawajatangaza ambao ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sita; William Ngeleja, Emmanuel Nchimbi, Mwigulu Nchemba, Stephen Wasira, Bernard Membe na Edward Lowasa.

Baadhi ya wanachama wa CCM na wanafunzi wa Vyuo Vikuu waliokuwepo wakati wa kutoa tamko hilo
Oscar Mwaihabi akitoa tamko kwa wanahabari, kwa niaba ya Wanazuoni mkoani Mbeya

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA