ASKARI MAGEREZA NA WA FFU WAKAMATWA NA NOTI BANDIA NA SARE ZA JWTZ


Naibu kamishna wa jeshi la polisi Mkoani Simiyu, Charles Mkumbo akiwaonesha waandishi wa habari baadhi ya sare za JWTZ ambazo zilikamatwa askari wa jeshi la polisi Mkoani Simiyu pamoja na Askari Magereza wilayani Bariadi

Jeshi la polisi mkoani Simiyu linawashikilia askari wawili wa jeshi la magereza na polisi kwa kukutwa na noti bandia ikiwa pamoja na sare za jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ).

Akitoa taarifa za kukamatwa kwa askari hao Kamanda wa polisi mkoani hapa Naibu Kamishina, Charles Mkumbo alisema kuwa askari hao walikamatwa juzi majira ya saa 9 mchana katika mtaa wa Old Maswa kata ya Nyakabindi Wilayani Bariadi.

Mkumbo Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni askari mwenye namba H 2420 PC Seleman Juma (25) ambaye ni askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Mkoani Simiyu, na askari namba B.6499 WDR Edmund Masaga (28) ambaye ni askari Magereza wilayani Bariadi.

Kamanda MkmMbo alieleza kuwa baada ya askari hao kukamatwa mmoja wao PC Selemani Juma alipopekuliwa katika mfuko wa suruali yake alikutwa na noti zingine za Bandia za elfu kumi kumi na jumla yake kama zingelikuwa halali zingelikuwa na thamani ya Shilingi 1,920,000.

Alisema kuwa askari hao walifika kwenye kibanda cha M-pesa kinachomilikiwa na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Old Maswa, Kassian Luhende (29) wakiwa na pikipiki yenye namba za usajili T 403 CXW aina ya Sunlg kwa lengo la kuweka fedha hizo kwenye simu.



Baadhi ya noti bandia walizokutwa nazo



Naibu kamishna wa jeshi la polisi Mkoani Simiyu Charles Mkumbo akiwaonyesha waandishi wa habari baadhi ya pesa bandia ambazo zilikamatwa askari wa jeshi la polisi




Sare zilizokamatwa.

CHANZO: WAVUTI.COM

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA