ATHARI ZA KUJITOA KATIKA FAO LA UZEENI
Makala hii imejumuisha mawazo ya wale wote waliochangia kwenye hoja ya haja juu ya dhana ya mifuko ya hifadhi ya jamii, niliyoiweka kwenye blog hii tarehe 31.07.2012. Asante kwa mawazo ya kujenga na kwa paomoja tuijenge Tanzania yetu. Natumaini tunaweza kukubaliana kuwa sera yoyote hupimwa ufanisi wake kwa kuzingatia inatekelezwaje mkabala na mahitaji ya uanzishwaji wake.Hakuna sera isiyokuwa na lengo, lengo likitimia ndipo tunapoweza kubaini kuwa sera imefaulu au imeshindwa. Dhana na lengo la mifuko ya hifadhi ya jamii ni kuwakinga wananchi ( wafanyakazi wa umma, binafsi, walioajiliwa na waliojiajili ) dhidi ya matukio yasiyo tarajiwa maana ambayo ni bayana. Lakini tukumbuke kuwa, neno “ jamii ” katika sera hii linatuvuta kuangaliazaidi ya mteja wa mifuko ya hifadhi ya jamii, lakini pia watu na taasisi zinazowazunguka ambazo kwa njia moja au nyingine huweza kuathiriwa na matendo ya mteja wa mifuko ya hifadhi ya jamii, hii ndio maana mifuko mingi ya hifadhi ya jamii huto