WALIMU WASHINIKIZA KUGOMA MKOANI MARA HAPO KESHO
- Get link
- X
- Other Apps
Shomari Binda,
Musoma
Chama cha walimu (CWT) Mkoa wa Mara kimewasihii walimu kutohadaika na
kauli ya Serikali ya lkuwataka kutokugoma kwani haki zao bila kuchua
hatua hutua hiyo hazitatimizwa kwa wakati.
CWT imesema
upatikanaji wa maslahi bora ya kazi yatapatikana kwa kushirikiana katika
mgomo utakaoanza kesho ili Serikali ione umuhimu wa madai yao ambayo
wamekuwa wakiyadai kwa muda mrefu sasa bila kupatiwa ufumbuzi.
Katibu wa CWT Mkoa wa Mara Fatuma Bakari amesema walimu wasiwe waoga
kutetea haki zao kwani mgomo huo huko kisheria na kinachofanywa na
Serikali ni vitisho kwao ambavyo amesema havina msingi.
Bakari
amewakumbusha walimu kuwa madai yao ya maslahi bora ni ya muda mrefu
huku akihituhumu Serikali kuendelea kuyapuuzia na kuwafanya kuishi
maisha duni na kifukara licha ya kufanya kazi kubwa nayakujituma.
Uchunguzi uliofanywa na BINDA NEWS Mjini Musoma umeonyesha kuwa mgomo
huo hupo kesho na walimu wengi wamenukuliwa wakisema wako tayari kugoma
ili kuishinikiza Serikali kutatua kero zao wanazozidai.
Walimu
hao wamesema kamwe hawawezi kuwasaliti viongozi wao wa Kitaifa
waliowachagua na kuwaachia vita hiyo ya madai ya msingi wapigane wenyewe
kama vile wanapigania maslahi yao binafsi.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment