KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MAMA YANGU GODRIVER POTI

LEO ni miaka mitatu imepita tangu mama yangu mzazi GODRIVER POTI alipotutoka duniani,kiukweli hii ni siku ambayo huwa siwezi kuisahau maishani mwangu,kwani nilimpoteza mtu aliyekuwa muhimu sana tena sana nadiriki kusema hivyo kwa kuwa ndiye aliyekuwa msatali wambele kuhakikisha watoto wake tunapata elimu bora,tunajengeka kimaadili kwa kuturekebisha pale tulipokuwa tukikosea lakini pia akusisita kutuonyesha njia iliyosahihi ya kufuata ili kuweza kufanikiwa kimaisha.

Pumzika kwa Amani mama huko uliko siku zoteza maisha yetu hapa duniani tunakukumbuka sana  na tunaamini kuwa siku moja tutaweza onana,Watoto wako Nyanja,Erick,Masatu,Jackqueline na Felister Tunakukumbuka sana tunakosa upendo wako..mama unakumbukwa na dada zako,marafiki na jamaa kwa ujumla.

          Upumzike kwa amani mama

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA