TWANGA PEPETA KUWAPA BURUDANI WAKAZI WA MUSOMA
Bendi ya Muziki wa Dansi ya Twanga Pepeta imepania kukonga nyoyo za wapenzi wa bendi hiyo na wapenzi wote wa Muziki Mjini Musoma siku ya Ijumaa ya Machi 31 pale watakapofanya onyesho lao la kwanza Mjini hapa baada ya kufanya hivyo takribani miaka 3 iliyopita. Akizungumza na mwakilishi wa blog hii kutoka Musoma Bwana Shomari Binda kwa njia ya simu wakiwa njiani kuja Musoma,mratibu wa ziara hiyo ambayo ni maalumu kwa wakazi wa Kanda ya ziwa Martin Sospeter amesema kuwa wamefanya maandalizi ya kutosha kwa muda wote ili kuhakikisha wanatoa burudani ambayo itakidhi haja kwa wale wote watakaobahatika kufika kuangalia onyesho la bendi hiyo. Amesema katika ziara hiyo wataitambulisha Album yao mpya inayokwenda kwa jina la Dunia Daraja ambapo ndani yake kuna nyimbo kama vile Mapenzi hayana kiapo,Penzi la Shemeji,Mtoto wa Mwisho pamoja na nyi ngine zilizomo katika Album hiyo. Martini amesema kuwa licha ya kupata Burudani ya nyimbo mpya za Bendi hiyo,wapenzi wa Twanga Pepet...