WABUNIFU WA MAVAZI NA WANAMITINDO KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE ONYESHO LA 'SOUTH AFRICA FASHION WEEK'


Millen Magese (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanamitindo na wabunifu watakaokwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki katika maonyesho ya 'South Africa Fashion Week'
WABUNIFUwatatu, Doreen Estazia Noni anayetumia Lebo ya eskado bird, Jamila Vera Swai na Evelyne Rugemalira wamepata nafasi ya kuchaguliwa kwenda kwenye maonyesho ya mitindo yajulikanayo kama South Africa Fashion Week nchini Afrika kusini kupitia kampuni ya Millen Magese Group company Limited.
Wabunifu hao watapanda jukwaani siku ya Aprili Mosi katika onyesho linalobeba jina la Tanzania International Fashion Exposé (TIFEX) by Millen Magese introducing Eskado Bird, Jamila Vera Swai and Evelyne Rugemalira. Millen alipata fursa ya kutembelea wabunifu hao na kujionea jinsi walivyokuwa wabunifu katika fani hiyo na kuhamasika kuwachukua na kushiriki katika maonyesho hayo maarufu ya mitindo katika bara la Afrika.
Alisema kuwa amevutiwa sana na jinsi walivyokuwa wabunifu na hivyo kuhamasika kuwapa nafasi hiyo ya kujitangaza kimataifa kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kupitia mradi huu anbao pia dhumuni lake kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kimataifa. Alifafanua kuwa mpango huu pia una lengo la kuitangaza Tanzania kupitia fani ya mitindo dunia nzima kama New York fashion week, London Fashion Week, Lagos Fashion week na Milan Fashion week.
Alisema kuwa hayo yanawezekana kutokana na uzoefu wake wa miaka nane katika fani ya mitindo na mahusiano mazuri kati yake wadau wa mitindo. Mbali ya wabunifu hao, Millen pia amewapa nafasi wanamitindo watatu, Anastazia Gura (21) na mapacha, Victoria Casmir (20) na Victor Casmir kuonyesha mitindo katika maonyesho hayo ya Afrika Kusini.
Wanamitindo hao wamepata nafasi hiyo baada ya kuwashinda wengine 486 waliofika katika usaili uliofanyika kwenye hotel ya Serena chini ya majaji, Mustapha Hassanali, Ritha Poulsen na mwanamitindo maarufu Aminat Ayinde kutoka kampuni ya America Next top model cycle 12.
Mbali ya wanamitindo hao Millen pia ameingia mkataba wa kufanya kazi na mwanamitindo wa kiume, Benard Chizi ambaye pia alishinda katika usaili huo na pia ataungana na wenzake kwenda Afrika Kusini. Millen pia alionyesha kusikitishwa na wanamitindo maarufu ambao walikuwa wanawasiliana naye akiwa Afrika Kusini kutaka kusaidiwa kufika hatua za kimataifa. Alisema kuwa cha kushangaza, wanamitindo hao, hawajajitokeza katika usaili huo na kumsononesha sana.
“Hii inaonyesha jinsi gani wanamitindo hao hawajiamini, usaili wangu ulikuwa fursa pekee ya wao kuonyesha vipaji vyao kimataifa, hata hivyo hawakufika, nawapongeza waliofika kwani wameonyesha kuwa wanania na ninaamini watafanya vyema huko Afrika Kusini,” alisema.
 Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Tabasamu Pr Consultancy
Email: tabasamupr@gmail.com, Mobile: 0754 602674, 0655 602674

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA