MANISPAA YA MUSOMA YAANDAA MIKAKATI YA KUBORESHA USAFI

Na Shomari Binda,
Musoma

Halimashauri ya Manispaa ya Musoma Mkoani Mara imeandaa mikakatia mbalimbali ya kuhakikisha Manispaa hiyo inakuwa katika hali ya usafi na kuwa miongoni mwa Miji misafi hapa Nchini kama ilivyokuwa katika Miaka ya nyuma.

Kauli hiyo imetolewa jana na Afisa wa Afya wa Manispaa ya Musoma Peter Mtaki Ofisini kwake alipokuwa akizungumza na BINDA NEWS kuhusiana na maandalizi ya uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa mazingira itakayoanza Machi 30.

Alisema moja ya mikakati ambayo wameipa kipaumbele ni pamoja na kusimamia Sheria ndogo ndogo za usafi wa Mazingira zilizotungwa mwaka 2010 ambazo bado zinaendelea kutumika hadi sasa lakini zimekuwa hazizingatiwi na Wananchi.

Mtaki alidai Sheria hizo zinamtaka kila mkazi kuweka eneo lake safi kuanzia majumbani,eneo lake la kazi na maeneo ya Biashara pamoja na kuchangia gharama za Usafi kama ada ya Usafi.

Alieleza kuwa Sheria hiyo inatamka kwa wale wanaokuwa wagumu wa kutojali usafi na kuchafua mazingira watatozwa faini ya shilingi 50,000/= au kifungo kisichozidi miezi 3 au adhabu zote kifungo na faini kwa pamoja.

"Katika kipindi cha nyuma Manispaa ya Musoma ilikuwa ni moja ya Miji Misafi hapa Nchini na Mwaka 2005 ilishika nafasi ya pili Kitaifa lakini kwa sasa tumeamua kusimamia kwa ukaribu zaidi Sheria hizi ili kurudisha hadhi ya Mji huu.

"Mji kama wa Moshi umeendelea kuonekana ni moja ya Miji misafi kwa kuwa wanafatilia kwa karibu na kusimamia Sheria ndogo ndogo ambapo hata mtu akitupa karatasi ya pipi anakutana na adhabu,"alisema Mtaki.

Alisema kampeni ya Usafi wa Mazingira inamtaka kila mtu awe ni mlinzi wa mwenzake na atakayeonekana anachafua Manzingira atua zichukuliwe papo hapo na kufikishwa kwa wahusika mitaani,katani au Manispaa kwa hatua zaidi.



Afisa huyo wa Afya wa Manispaa ya Musoma aliongeza kuwa wameahidi kumuenzi Makamo wa Rais Dr.Mohamed Gharib Bilal alipofanya uzinduzi wa Kampeni ya Usafi wa Mazingira Kitaifa Februari 2011 katika Miji,Manispaa na Majiji hapa Nchini kwa kufanya zoezi hilo kuwa endelevu kufanya Usafi kila Ijumaa ya mwisho wa Mwezi

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA