TWANGA PEPETA KUWAPA BURUDANI WAKAZI WA MUSOMA
- Get link
- X
- Other Apps
Bendi
ya Muziki wa Dansi ya Twanga Pepeta imepania kukonga nyoyo za wapenzi
wa bendi hiyo na wapenzi wote wa Muziki Mjini Musoma siku ya Ijumaa ya
Machi 31 pale watakapofanya onyesho lao la kwanza Mjini hapa baada ya
kufanya hivyo takribani miaka 3 iliyopita.
Akizungumza na mwakilishi wa blog hii kutoka Musoma Bwana Shomari Binda
kwa njia ya simu wakiwa njiani kuja Musoma,mratibu wa ziara hiyo
ambayo ni maalumu kwa wakazi wa Kanda ya ziwa Martin Sospeter amesema
kuwa wamefanya maandalizi ya kutosha kwa muda wote ili kuhakikisha
wanatoa burudani ambayo itakidhi haja kwa wale wote watakaobahatika
kufika kuangalia onyesho la bendi hiyo.
Amesema katika ziara
hiyo wataitambulisha Album yao mpya inayokwenda kwa jina la Dunia Daraja
ambapo ndani yake kuna nyimbo kama vile Mapenzi hayana kiapo,Penzi la
Shemeji,Mtoto wa Mwisho pamoja na nyingine zilizomo katika Album hiyo.
Martini amesema kuwa licha ya kupata Burudani ya nyimbo mpya za Bendi
hiyo,wapenzi wa Twanga Pepeta pia watapata ladha ya vibao vya zamani vya
Bendi hiyo vilivyopata kutamba ambavyo vitaongozwa kuimbwa na
mwanamuziki mkongwe hapa nchini ambaye amejiunga tena na bendi hiyo
Mwinjuma Muumini(Kocha wa Dunia).
Amesema kuwa licha Muumini na
wanamuziki wengine wa bendi hiyo wameongozana na mshindi wa kwanza wa
mashindano ya Bongo Star Sarch (BSS)mwaka 2011 Haji Ramadhani ambaye pia
ampania kutoa burudani ya kutosha kwa wakazi wa Musoma ikiwa kama
shukrani ya kumpigia kura na kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano
hayo yaliyowakutanisha mastaa kibao.
Ameongeza kuwa burudani
hiyo ya Twanga Pepeta itafanyika katika ukumbi wa Musoma Club kwa
kiingilio cha shilingi elfu kumi (10,000) huku burudani hiyo ikipangwa
kuanza majira ya saa2 usiku a tayari maandalizi yote katika ukumbi huo
yamekwisha kukamilika na kinachosubiliwa ni kwa wapenzi wa bendi hiyo
kwenda kulicheza Twanga.
habari imeandaliwa na mwakilishi wa blog hii kutoka Musoma Bwana Shomari Binda.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment