HUDUMA MPYA YA KISASA INAYOKUUNGANISHA MTANDAO WA MICHUZI BLOG BURE
Tovuti
yako uipendayo inakupa huduma ya kujivinjari bure kutoka Uhuruone
Muhidini
Issa Michuzi akishikiriana na Uhuruone wanawapatia wakazi wote wa Dar es Salaam
huduma ya “Wifi hotspots” ambayo itawapa wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya
bure ya kutembelea tovuti ya Michuzi.
Kwa kupitia mitambo yao ya “Wifi Mesh”
iliyopo Dar es Salaam ambayo imeunganishwa na tovuti ya Michuzi,wakazi wa Dar
es Salaam wanatangaziwa kwamba wawashe kompyuta zao na kuunganishwa na taarifa
za punde bila gharama yoyote.
Akikaririwa
katika mahojiano ndugu Issa Michuzi alisema hivi, “Ni mapinduzi ya kweli ambapo
Watanzania wanachukua hatua katika kuleta taarifa mbalimbali kwa wananchi
katika viwango nafuu.
Ninaamini hii itaongeza mawasiliano kwa watu wetu na ni
ndoto yangu kwamba tovuti ya Michuzi itakua huru kufika kwa Watanzania wote
hivi karibuni”.
Akiwa
ofisini Bwana Rajabu Katunda alisema, “Uhuruone imejikita katika kutoa huduma
kwa jamii na tumegundua kwamba taarifa za kijamii zinatakiwa kuwafikia
wanajamii kwa urahisi.
Tovuti nyingi zinatembelewa na Watanzania waliopo nchi
za nje kuliko wananchi waliopo nchini na hii siyo haki.
Kama nina uwezo kupata
taarifa kwenye tovuti ya Michuzi ni jukumu letu kama kampuni kuwawezesha
watanzania waliopo nchini pia kupata huduma.
Watanzania tunatakiwa kuwa na
utamaduni wa kusaidiana na kupeana moyo na hii itasaidia kukuza uchumi wetu sio
tu kununua na kuuza bidhaa kutoka nje.
Kwa
pamoja Bwana Michuzi na Katunda wamesema huu ni mwanzo tu na wanaamini kwamba
hili wazo litafuatwa na wengine. Kwa msisitizo Bwana Michuzi aliongea “Lazima
tuonyeshe mfano kwa vitendo sio maneno tu.
Tumechukua hatua ya kwanza katika
kufanikisha ndoto, wengine wanatakiwa kujiunga kwenye mapinduzi haya na
kufanikisha”
Kutembelea
tovuti ya Michuzi bila gharama washa Wifi kwenye Ipad, Tablet, Simu au Laptop.
Tafuta Michuzi blog Wifi, Unganisha ,fungua browser yako uipendayo mfano
Chrome, Internet Explorer, Safari au Firefox na nenda kwa Issa
Michuzi.blogspot.com.
Kama hautaona tovuti ya Michuzi Wifi, tafadhali
wasiliana na Uhuruone kwa email ifuatayo, issa.michuzi@uhuruone.com au piga simu namba 255779477477 ili uweze
kuunganishwa
Comments
Post a Comment