Posts

WAZIRI MKUU AHITIMISHA MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAA KITAIFA KATIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA

Image
 Wazi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akikabidhi zawadi ya cheti mshindi wa kwanza wa jiji lililofanya vizuri kwenye maonyesho hayo kwa mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe.  Waziri mkuu mh. Pinda akiwa ameongozana na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Ndikilo alipata fursa ya kutembelea mabanda ya maonyesho hayo toka halmashauri mbalimbali nchini zilizoshiriki.  Watumishi wa ofisi ya TAMISEMI wakiwa kwenye banda la maonyesho la ofisi hiyo katika viwanja vya CCM Kirumba wakisubiri kutoa maelezo kwa waziri mkuu ambaye alipita kutembelea mabanda ya maonyesho.  Picha ya mchoro wa Jengola kisasa la kliniki ya wajawazito na watoto lililokwisha anza ujenzi wake katika eneo la mtaa wa Utemini jijini Mwanza ambalo likikamilika ujenzi wake litakuwa na taswira hii. Jengo hili litakuwa mbadala wa jengo ambalo linatarajiwa kuvunjwa la Kliniki ya zamani  lililopo mtaa wa barabara ya Makongoro. kupisha ujenz...

ASANTENI WADAU KWA KUNIPA USHINDI

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jambo ambalo linatokea katika maisha yangu kila kukicha,pia na kuwashukuru Ndugu,jamaa na marafiki walioko katika mtandao wa facebook kwa kuweza kunipigia kura za kutosha na kuweza kufanikisha kuibuka mshindi katika shindano la kutafuta blog bora za kitanzania ambalo limefanyika zaidi ya miezi 2 katika kupata washindi. Shindano hili linaratibiwa na website ya www.tanzanianblogawards.com ambayo ilianzishwa mwaka jana na mwaka huu shindano  limefanyika kwa mara ya pili likiwa na nia ya kuweza kutangaza blogs mbalimbali ambazo zinamilikiwa na watanzania waliopo nchini na wale waishio ng'ambo lakini pia kuweza kuwathamini kwa kile wanachokifanya katika kuhabarisha jamii kwaa ujumla. Shindano ili lilianza miezi 2 iliyopita kwanza kwa kuweza kunominate blog ambayo inafaa kuingia katika category mbalimbali ambazo zilikuwa zimeanishwa na waratibu,kwa mwaka huu zaidi ya blog 600 za kitanzania zilipendekezwa kuingia katika shindano hili na...

BBM PARTY 2012 @Mbalamwezi Beach

Image

WALIOCHAGULIWA KUFANYA USAILI WA POLISI HADHARANI

Na Thomas Dominick Musoma JESHI la Polisi Mkoa wa Mara limetoa majina ya vijana ambao wamechaguliwa kwa ajili ya kufanya usaili wa kujiunga na jeshi hilo ambapo kanda ya ziwa utafanyika Julai 2 hadi 4 mwaka huu katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza. Akizungumza na waaandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Absalom Mwakyoma alisema kuwa majina hayo yatabandikwa kwenye mbao za matangazo zilizopo katika ofisi za Mkoa na wilaya zote. “Mwaka huu tumeamua kuchukua vijana watakaojiunga na jeshi letu kutoka mashuleni ambao wamemaliza kidato cha nne mwaka jana na cha sita mwaka huu hivyo tunawaamba vijana wote waende wasome na wajue kama jina lake lipo katika orodha yetu,” “Hii tumerahisisha ili kupunguza msongamano wa vijana kufika katika ofisi zetu na kuulizia ajira hizo na kama unatumia mtandao tafuta katika mtandao wetu wa www.policeforce.go.tz na utaona jina lako na vituo vya usaili,”alisema. Alisema kuwa vijana ambao ...

TANESCO YATANGAZA NEEMA KWA WATEJA

 SHIRIKA la Umeme Tanzania(Tanesco), limesema ifikapo kesho litakuwa limeshawaunganishia umeme wateja wake wote walioomba kupata huduma hiyo kwa muda mrefu. Hayo yalisemewa jana na meneja uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Alisema kwa sasa shirika hilo lina vifaa vya kutosha na kwamba ndicho kitu ambacho kilikuwa kikiwakwamisha kutekeleza majukumu yao. “Mteja wetu yeyote ambaye ameomba anapaswa kuwa ameunganishiwa umeme ifikapo Juni 30, mwaka huu,”alisema Badra. Alisema wateja ambao walikuwa wameomba wafike katika ofisi za Tanesco katika maeneo yote zilizopo ofisi zao ili waweze kupatiwa huduma hiyo. “Tutatoa namba maalum ili wateja ambao watakuwa wanasumbuliwa na wafanyakazi wetu waweze kutupigia moja kwa moja na sisi tutashughulika nao,”alisema.

KUWAONA YANGA V EXPRESS J'MOSI TAIFA BUKU TATU TU

Image
WAKATI mabingwa wa ligi kuu soka nchini Uganda,  Express wakiwasili leo tayari kwa mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Yanga, kiingilio cha juu cha mchezo huo utakaoipgwa jumaosi katika uwanja wa Taifa kimepangwa kuwa shilingi 20,000 kwa VIP A. Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu amesema kwamba mashabiki watakaokaa VIP watalipa shilingi, 15,000 kwa VIP B na C ,shilingi 5,000 ni kwa watakaokaa biti vya  kijani na wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na chungwa watalipa shilingi 3,000. source  http://dinaismail.blogspot.com/

VODACOM KUWAZAWADIA MABINGWA WA LIGI KUU BARA J'MOSI

Image
         Simba Sc ndiyo mabingwa wa VPL         AZAM FC (washindi wa pili)            Yanga SC (Washindi wa tatu) John Bocc wa Azam FC (Mfungaji bora wa VPL) Kampuni ya Vodacom itakabidhi zawadi kwa washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu 2011/2012 katika hafla itakayofanyika Juni 30 mwaka huu kwenye hoteli ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam.   Hafla hiyo itakayohudhuriwa na wawakilishi wawili kutoka katika klabu ya Ligi Kuu itaanza saa 12 jioni. Katika hafla hiyo washindi mbalimbali wakiwemo bingwa, makamu bingwa na mshindi wa tatu.   Wengine watakaozawadiwa ni mfungaji bora, kipa bora, timu bora yenye nidhamu, mchezaji bora wa ligi, refa bora na kocha bora.   Chanzo http:// dinaismail.blogspot.com