ASANTENI WADAU KWA KUNIPA USHINDI

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila jambo ambalo linatokea katika maisha yangu kila kukicha,pia na kuwashukuru Ndugu,jamaa na marafiki walioko katika mtandao wa facebook kwa kuweza kunipigia kura za kutosha na kuweza kufanikisha kuibuka mshindi katika shindano la kutafuta blog bora za kitanzania ambalo limefanyika zaidi ya miezi 2 katika kupata washindi.

Shindano hili linaratibiwa na website ya www.tanzanianblogawards.com ambayo ilianzishwa mwaka jana na mwaka huu shindano  limefanyika kwa mara ya pili likiwa na nia ya kuweza kutangaza blogs mbalimbali ambazo zinamilikiwa na watanzania waliopo nchini na wale waishio ng'ambo lakini pia kuweza kuwathamini kwa kile wanachokifanya katika kuhabarisha jamii kwaa ujumla.

Shindano ili lilianza miezi 2 iliyopita kwanza kwa kuweza kunominate blog ambayo inafaa kuingia katika category mbalimbali ambazo zilikuwa zimeanishwa na waratibu,kwa mwaka huu zaidi ya blog 600 za kitanzania zilipendekezwa kuingia katika shindano hili na ni blog tano tu zilizotakiwa kuingia katiaka category moja,jumla ya category 15 mwaka huu ndio zilizokuwepo,hivyo blog yetu hii www.nyanja.blogspot.com ikapendekezwa na ninyi wadau wenyewe na ikaweza kuingizwa katika category ya BEST FAMILY/PERSONAL BLOG na kuweza kuibuka na ushindi wa kishindo kabisa wa 70.35% wakati mshindani mwingine anayenifuta akipata 12% hivyo mdau mwenyewe unaona ni kwa jinsi gani kura yako imeweza kufanikisha kwa kiasi kikubwa kuleta ushindi huu.

Ushindi huu si wangu tu bali na ninyi wadau pia kwani ndio mnanipa moyo zaidi wa kuweza kufanikisha plans zangu ambazo ninazo ambazo naona kabisa tayari ndoto ambayo nilikuwa nikiziota sasa zinaanza kukamilika taratibu kwani umekuwa mwanzo mzuri sana kwa mwaka huu..

Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kabisa kwa watu hawa kwanza ni Rashidi B.Jumaa, Francis Moses aka Creator, Hassan Mrope, Lucky Mgimba, Lizzy Dommy,Victor Nivox, Lilian Kaswamila,Naima Abasily,Omary A. Mchecheto, Loveness Dickson, Abdul Abdallah,cousin wangu Dickson Philipo,Makongo Charles , Daniel Aloyce, Malfred Alfred, Paul Mnyamwezi, Ticha  Kinye,Josefly, Emmanuel Mallewo, Malare Murilo, Anthonius Clement, Fidius Kalekezi, Anania Komba, Wilhelm Oddo, Steve Zakaria, Ramadhani Juma,Robert Latonga,Kelvin Majura,Mzee Mandala,Chacha O. Wambura,Raheem Keissie,Barley Zabron, Jailesi Massimbo,Joseph Simon,brother Mlawa Isihaq na wengine wengi kama jina lako sijalitaja basi usijisikie vibaya tuko pamoja sana kiukweli ni watu wengi sana ambao wanaongoza harakati hizi mpaka zinafanikiwa, lakini pia natoa shukurani zangu za dhati kabisa kwa wanafunzi wenzangu wa chuo kikuu cha mt.Augustino kwa ushirikiano wao ,wanadarasa wenzangu BAPRM students, Musomians members,SSPRA members pia bloggers wote Tanzania bila kumsahau brother GSENGO,Djchoka, Sina cha kuwalipa ndugu zangu lakini I appreciate for your support.

                                                         THANK U.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA