WAZIRI MKUU AHITIMISHA MAADHIMISHO YA SIKU YA SERIKALI ZA MITAA KITAIFA KATIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA


 Wazi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akikabidhi zawadi ya cheti mshindi wa kwanza wa jiji lililofanya vizuri kwenye maonyesho hayo kwa mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe.

 Waziri mkuu mh. Pinda akiwa ameongozana na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Ndikilo alipata fursa ya kutembelea mabanda ya maonyesho hayo toka halmashauri mbalimbali nchini zilizoshiriki.

 Watumishi wa ofisi ya TAMISEMI wakiwa kwenye banda la maonyesho la ofisi hiyo katika viwanja vya CCM Kirumba wakisubiri kutoa maelezo kwa waziri mkuu ambaye alipita kutembelea mabanda ya maonyesho.

 Picha ya mchoro wa Jengola kisasa la kliniki ya wajawazito na watoto lililokwisha anza ujenzi wake katika eneo la mtaa wa Utemini jijini Mwanza ambalo likikamilika ujenzi wake litakuwa na taswira hii. Jengo hili litakuwa mbadala wa jengo ambalo linatarajiwa kuvunjwa la Kliniki ya zamani  lililopo mtaa wa barabara ya Makongoro. kupisha ujenzi wa jengo la Benki kuu ya Tanzania litakaloshughulikia mikoa ya kanda ya Ziwa na Magharibi.

 Hii ni moja ya michoro ya ramani na muonekano wa baadhi ya barabara za jiji la Dar es salaam ambazo zitatoa huduma ya usafiri wa mabasi maalum ya abiria ili kupunguza msongamano na adha ya usafiri kwa jiji hilo.

 Moja ya jengo ya kisasa ambalo limeanza kujengwa katika eneo la nyuma zilipo ofisi kuu za Halmashauri ya jiji la Mwanza (Idara ya Afya).

 Kushoto Waziri mkuu mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa afisa mipango miji wa jiji la Mwanza bw. Maduhu jinsi muonekano wa jiji la Mwanza litakavyokuwa ifikapo mwaka 2025 ikiwa ni moja ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya makazi, uwekezaji na ukamilishwaji wa majengo ya kisasa katikati ya jiji na pembezoni ya jiji la Mwanza.
 Kikosi cha askari wa mbwa ambao pia kimekuwa ni kivutio kwenye maonyesho hayo.

Waziri mkuu akipata maelekezo ya kina toka kwa afisa wa maliasili wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema alipofika katika banda hilo.
Waziri mkuu akipigwa butwaa na kusitisha hotuba yake kwa dakika takribani tatu ili kusoma ujumbe wa mkazi wa jiji la Mwanza bwana Sikitu 'Mandela' kama unavyosomeka hapo chini ambapo kwa upande wa pili ujumbe ulisomeka "TURUDISHIENI RELI YETU YA KATI".
Ni moja kati ya wakazi wa jiji la Mwanza bwana Sikitu maarufu kwa jina la Mandela akifikisha ujumbe wake kwa waziri mkuu Mizengo Pinda wakati akihutubia kwenye kilele cha maadhimisho hayo.
source www.gsengo.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA