TANESCO YATANGAZA NEEMA KWA WATEJA

 SHIRIKA la Umeme Tanzania(Tanesco), limesema ifikapo kesho litakuwa limeshawaunganishia umeme wateja wake wote walioomba kupata huduma hiyo kwa muda mrefu.

Hayo yalisemewa jana na meneja uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Alisema kwa sasa shirika hilo lina vifaa vya kutosha na kwamba ndicho kitu ambacho kilikuwa kikiwakwamisha kutekeleza majukumu yao.
“Mteja wetu yeyote ambaye ameomba anapaswa kuwa ameunganishiwa umeme ifikapo Juni 30, mwaka huu,”alisema Badra.

Alisema wateja ambao walikuwa wameomba wafike katika ofisi za Tanesco katika maeneo yote zilizopo ofisi zao ili waweze kupatiwa huduma hiyo.

“Tutatoa namba maalum ili wateja ambao watakuwa wanasumbuliwa na wafanyakazi wetu waweze kutupigia moja kwa moja na sisi tutashughulika nao,”alisema.



Alisema hakuna mfanyakazi wa Tanesco anayepaswa kumzungusha mteja wa shirika hilo hivyo mteja yeyote atakayezungushwa awasiliane na makao makuu ili waweze kushughulikiwa.

Katika hatua nyingine Tanesco imesema  wanatarajia kuzindua mtambo wao mpya wa megawati 100 unaoiwa Jacobsen.

Badra alisema mtambo huo utazinduliwa kesho na kwamba ongezeko la megawati hizo 100 utafanya nchi iwe na megawati 800 za umeme.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA