viwango vipya vya soka.... Brazil yashuka
* Hispania yashika ukanda, Tanzania yazidi kuzama ZURICH, Uswisi BRAZIL imeporomoka kwa nafasi mbili kwenye ubora wa viwango vilivyotolewa jana na Shirikisho la Soka la Kimataifa, FIFA, huku Hispania ikishika ukanda ikifuatiwa na Uholanzi. Mabingwa hao wa dunia mara tano, walikuwa wakishika namba moja kwenye chati hizo za FIFA tangu April 2010 imeporomoka ikiwa ni baada ya matokeo mabaya ya Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Afrika Kusini. Brazil iliondoshwa na Uholanzi katika mechi ya robo fainali kwa kufungwa mabao 2-1 ambayo ilikuwa ikishika nafasi ya nne kabla ya kupanda nafasi ya pili kwenye viwango hivi vipya vya Fifa. Uholanzi ilifungwa bao 1-0 na Hispania kwenye fainali. Kwa mujibu wa viwango hivyo vipya vya Fifa, Tanzania imeshuka kwa nafasi nne kutoka nafasi ya 108 ambayo ilikuwa ikiishikilia mwezi Aprili mpaka nafasi ya 112. Januari mwaka huu, Tanzania ilikuwa nafasi ya 108 sawa na Februari kabla ya kushuka kwa nafasi moja hadi 109 mwezi Machi. Ilipanda tena kwa nafasi