REDNAPP HADI MWAKA 2013


Redknapp

Meneja wa klabu ya Tottenham Harry Redknapp ameongeza mkataba wa kuendelea kukinoa kikosi cha klabu hiyo mpaka mwaka 2013.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 63 ameongeza mkataba huo huku akiwa ameifanyia makubwa klabu hiyo ambayo msimu ujao itashiriki kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Hatua hiyo ya kuamiliwa na mabosi wake na kupewa mkataba mpya imemkuna sana Harry Redknapp ambae anadai huenda imeshababishwa na utawala mzuri alionao katika kikosi chake ambapo mara kadhaa amekua akiwaeleza ukweli wachezaji wake.

Kabla ya kusaini mkataba mpya, mkataba wa zamani wa miaka miwili wa Harry Redknapp ulikuwa unatarajia kufikia kikomo mwaka ujao.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA