Posts

mtoto wa kitaa kutoka TMK akiwa na wakitaa mwenzie kutoka Brooklyn

miss Mara afunika miss lake zone

Image
HUYU NDIYE VODACOM MISS LAKE ZONE 2010 FATMA IBRAHIM KUTOKA MUSOMA ALIYESHINDA KATIKA KINYANG'ANYIRO KILICHOFANYIKA USIKU WA KUAMKIA LEO NDANI YA KIWANJA KIPYA KABISA HUJAWAHI TIA MGUU, NATILO HOTEL JIJINI MWANZA. KUTOKA KUSHOTO MSHINDI WA TATU VODACOM MISS LAKE ZONE 2010 BUDURI IBRAHIM NA KULIA KABISA MSHINDI WA PILI MAGRET GODSON KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MISS LAKE ZONE 2010 FATMA IBRAHIM(KATIKATI). KWA MUJIBU WA KANUNI ZA MISS TANZANIA WOTE HAWA WAMEINGIA KATIKA MCHAKATO WA FAINALI ZA KUMTAFUTA MISS TANZANIA. picha ni kwa hisana ya blog ya gsengo

USIKU WA FIESTA ULIVYOFUNIKA HAPA DAR

Image
Lil Kim baada ya kupiga songi zake kadhaa,alimuita msanii Juma Nature jukwaani na kuanza kuimba nae,ama kwa haki kuliibuka makelele na mayowe ya shangwe ile mbaya uwanjani hapa. Vijana wa kundi la Bracket toka Nigeria wakikupa 'Yori Yori' Mkali wa aladji aladji kutoka Ivory Coast,Jeff akimchezesha densa wake na kibao chake maarufu kabisa cha aladji mbele ya umati mkubwa uliofika kwenye tamasha la fiesta jipanguse. Kundi la Wanaume TMK,Chege,Temba na Kr Mulla wakilivamia jukwaani vyema kabisa na moja ya wimbo wao wa Mambo bado,Makelele yalitawala hapa uwanjani ile mbaya ni full . Ni barnaba na Lina hawa pia walipangawisha mbaya na kibao chao cha wrong no Mkali Roma on the stage,huyu jamaa nilikuwa sijawai kumuona on the stage lakini kitu nilichokiona ni kwamba jamaa ni mkali sana,watu walinyanyua mikono yao kumpa support ya kutosha. Umati wa watu uliojitokeza kwenye usiku wa fiesta Mambo ya aladji ,hawa madensa wanakata viuno ni hatari Lil kim on the stage Lil kim pia ali

KUTANA NA WATU WAPYA,INASAIDIA.

Image
Kwa walio wengi kukutana na kupata nafasi ya kujua watu wapya ni raha sana.Ila kuna wengine huona ni kupoteza muda,hujisikia hayuko huru hasa kama huyo mtu anamuuliza maswali au kumuongelesha.Ila kuna faida kubwa ya wewe kujipa nafasi ya kukutana na kufahamiana na watu wapya mara kwa mara. Urafiki.. · Kukutana na watu wapya kunaweza kukuongezea marafiki.Hali ambayo inakusaidia kiakili na kimwili .Mtu mpya anaweza kukufundisha kitu kipya ambacho wewe ulikuwa hujui,kukupeleka mahali ulikuwa hujawahi kwenda,kula chakula ambacho ulikuwa hujawahi kula n.k Kujifunza · Kukutana na watu wapya kunakusaidia kujifunza vitu vipya.Ukikutana na mtu mpya utajifunza vitu vipya,mbinu mpya za kufanya jambo fulani,lugha mpya,au kuweza kukupa njia ya kutatua tatizo Fulani kwenye maisha.Ukichukua muda kumjua mtu inaweza kukusaidia kuongeza wigo wako wa ufahamu na kujua mbinu mpya katika maisha. Uelewa · Kukutana na watu wapya kunakupa nafasi ya kuelewa tamaduni tofautitofauti imani,wanavyoishi,wanachothami

FANYA MAZOEZI MAPEMA YA RAAAAAAAAAAA

Verse 1: Lil' Kim I Come From Bed-Stuy, Where Niggas Either Do Or They 'gon Die gotta Keep The Ratchet Close By someone Murdered, Nobody Seen Nobody Heard It, Just Another Funeral Service niggas Will Get At You, Come Through Shinin They Yap You, In Broad Daylight Kidnap You thugs They Get Clapped To, Police Stay On Us Like Tatoos, Niggas Only Grind Cause We Have To money Is Power, Sling Crack, Weed And Powder, Fiends Come Through Every Hour it's All About That Dollar, And We No Deal With Cowards, Weak Lamb Get Devoured by The Lion And The Concrete Jungle The Strong Stand And Rumble the Weak Fold And Tumble If They Land Up Trouble brooklyn Home Of The Greatest Rappers, Big Comes First And The Queen Comes After chorus: Lil' Kim now Put Your Lighters Up, Bed-Stuy, Put Your Lighters Up fort Greene, Put Your Lighters Up, Flatbush Keep Puttin Them Lighters Up brownsville, Put Your Lighters Up, East New York, Put Your Lighters Up bushwick Keep Puttin Them Lighters Up, No Matte

watakao pagawisha siku ya Fiesta DAR

Image
Bracket LIL KIM Kundi la Wanamuziki kutoka nchini Nigeria wajulikanao kwa jina la Bracket ,ambao wanatamba na nyimbo zao kadhaa ikimwemo ile ya yori yori and no time,pia watakuwepo COUPER DECALER kutoka IVORY COAST na kitu cha Aladji kutikisa ndani ya viwanja vya Leaders.........jipanguse rhaaaaaaaaaaaaaa

IMEKAA VIPI HII

Image
KAZI KWENU WADAU

KUTANA NA VICHWA HV NDANI YA VICTORIA FM- MUSOMA 90.6

Image
KAMA NI MARAFIKI WA UKWELI NDO HAWA WAPATE UWAPO KANDA YA ZIWA, MKOA WA MARA KATIKA MASAFA YA 90.6 NI VICTORIA FM, KUTOKA SHOTO LADY MARIA MGABO, ISABELA MSHANA , PASCHAL MICHAEL BUYAGA NA CARES ONE . NI MOTO BALAAA ! augustino picha ni kwa hisani ya blog ya www.gsengo.blogspot.com

Arusi ya Alicia Keys na Swizz Beatz ilifanyika Wikiendi

Image
Alicia Keys na Swizz Beatz Hatimaye ule uhusiano wa tangu mwaka 2008 kati ya mwanamuziki wa Marekani bi. Alicia Keys na mtayarishaji wa muziki Kasseem Dean aka Swizz Beatz umezaa ndoa mwishoni mwa wiki Alicia Keys na Swizz BeatzHafla ya ndoa hiyo ilifanyika kwa faragha kubwa siku ya Jumamosi katika eneo ambalo halijatajwa. Alicia Keys, miaka 29, amewahi kujishindia tuzo mbalimbali 12 za Grammys tangu kutoa albamu yake ya kwanza Songs in A Minor mwaka 2001. Dean, miaka 31, ambaye ana watoto wawili kutoka ndoa yake ya mwanzo, ameandika na kutayarisha nyimbo za wasanii zilizovuma sana akiwemo Beyonce na mumewe Jay-Z. Alicia Keya aliimba katika sherehe za ufunguzi za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi Juni, 2010.

Vigogo wazidi kubwagwa CCM

MATOKEO ya kura za maoni kwa nafasi za ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) yamezidi kutolewa nchini huku yakiwatupa nje ya bunge baadhi ya waliokuwa wakishikilia majimbo mbalimbali, jambo linaloashiria kuwa bunge lijalo litakuwa na sura nyingi mpya. Mkoa wa Dar es Salaam Katika Mkoa wa Dar es Salaam walioibuka kidedea na kuwamwaga wapinzani ni, Dkt. Makongoro Mahanga Jimbo la Segerea (2,148) akifuatiwa na Bw. Joseph Kessy (1,435), Jimbo la Ukonga aliyeoongoza katika matokeo ya awali ni Bi. Eugen Mwaiposya (1,885) akifuatiwa na Bw. Godwin Barongo (1,394), Jimbo la Kinondoni aliyeongoza ni Bw. Iddi Azan) akifuatiwa na Bi. Shy-Rose Bhanji, Jimbo la Ubungo aliyeibuka mshindi ni Bi. Hawa Ng'umbi ambaye amewamwaga Bw. Nape Mnauye na Bi. Shamsa Mwangunga. Mkoa wa Dodoma Mkoani ambao umetoa matokeo ya awali katika majimbo yote na matokeo hayo yanaweza kubadilika mara baada ya kukamilika kuhesabiwa kura katika vituo vyote. Jimbo la Dodoma Mjini Bw. Peter Chiwanga (3,183), Bw. David Mal

CHADEMA wampitisha Mbilinyi kuwania ubunge

Image
JOSEPH MBILINYI MWANAMUZIKI wa kizazi kipya nchini, Bw. Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Mr.II jana aliibuka kidedea kuwa mgombea ubunge Jimbo la Mbeya mjini baada ya kuwashinda mhandisi wa mitambo ya simu, Bw. Daud Mponzi na mwandishi wa habari wa Tanzania Daima, Bw. Christopher Nyenyembe. Katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Kiwira Motel ulishirikisha wapiga kura 362 kutoka katika kata zote 36 wa jijini Mbeya. Mwanamuziki huyo alishinda kwa kura 175 akifutiwa na Bw. Daud Mponzi aliyepata 122, mwandishi wa habari mndawamizi wa Tanzania Daima, Bw. Christopher Nyenyembe kura 54 na mwanaharakati Gwakisa Mwakasendo aliyeambulia kura 9. Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa, Bw. Sambwee Shitambla aliwataka wanachama wa chama hicho kuhakikisha wanachagua mgombea atakayeweza kukiuza chama hicho kupambana na CCM na hatimaye kushinda jimbo hilo. Alisema kuwa chama hicho hakitaki mgombea atakayepita kwa mbinu za kifisadi kama ilivyo kwa wagombea wengi wanaodaiwa kufan

Kocha Stars aja leo, kuanzia kibarua

KOCHA mpya wa Taifa Stars, Jan Poulsen anatua nchini leo kuanza kibarua chake kipya ambacho kitaanzia rasmi Cairo, Misri dhidi ya mabingwa wa Afrika, Mafarao, Agosti 11. Poulsen, raia wa Denmark atawasili nchini leo usiku kuinoa Stars iliyoachwa na Marcio Maximo aliyemaliza muda wake mwanzoni mwa mwezi. Kulingana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mechi hiyo ambayo ni ya kirafiki ya kimataifa ilipangwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa,Fifa. Ofisa Habari waTFF, Florian Kaijage, alisema jana kuwa baada ya kuwasili nchini Poulsen atakuwa na jukumu la kuanza mchakato wa kuteua wachezaji wa Stars na kuwaandaa kwa mechi hiyo siku kumi baadaye. Kaijage alisema kuwa ni matarajio ya shirikisho hilo kuwa mechi hiyo itakuwa sehemu muhimu ya matayarisho ya Stars kuanza harakati za kusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2012 zitakazoandaliwa kwa pamoja na Gabon na Guinea ya Ikweta. "TFF imekuwa ikifanya jitihada kubwa kuhakikisha St