UCHAGUZI MKUU 2010: Mawaziri wanyakua ushindi mezani
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimezidi kujitwalia majimbo ya ubunge kabla ya upigajikura hapo Oktoba 31 mwaka huu, baada ya idadi ya wagombea wake wakiwemo mawaziri kupita kwa ushindi wa 'mezani' wa mapingamizi dhidi ya washindani wao na kuwezesha chama hicho, kuweka kibindoni majimbo 16 hadi sasa hivi. Hadi jana, CCM iliweza kujitwalia majimbo zaidi likiwemo Mlele kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, baada ya mgombea wa CUF Abasi Rashid, kujitoa kwenye mbio hizo huku katikia Jimbo la Mtama, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akipita kwa mlango huo wa pingamizi dhidi ya Isaya Ndaka wa TLP, baada ya kukosa idadi ya wadhamini wanaohitajika. Kasi hiyo ya CCM ilizidi kuongezeka jana baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha kupita kwa mlango huo wa pingamizi dhidi ya mshindani wake kutoka Chadema Wenje Ezekie huku Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja, naye akipeta. Hadi sasa wana CCM waliotangazwa kuteuliwa wabunge na majimbo yao kwenye mabano ni