Watanzania wanaoishi nje hawatapiga kura 2010

Serikali imesema kuwa bado haijakamilisha mkakati utakaowezesha Watanzania wanaoishi nje ya nchi kupiga kura hivyo watakosa haki hiyo katika uchaguzi mkuu utakoafanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe alisema kuwa, kwa sasa bado wanalishughulikia suala hilo lakini hawawezi kupiga kura kwa sababu mchakato huo bado.

“Hawawezi kupiga kura watanzania wanaoishi nje ya nchi, kwa sababu suala lao bado linafanyiwa kazi, hivyo basi hawawezi kupata nafasi ya kushiriki kwenye uchaguzi huu,”alisema Membe jana alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, Serikali bado inaendelea kuweka mazingira yatakayowezesha watu hao kupiga kura waweze kushiriki katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Alisema pindi mchakato huo utakapokamilika, Serikali itaweka hadharani ili wadau wote wafahamu namna utakavyotekelezwa kwa kuweka mazingira huru yenye lengo la kupanua demokrasia.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA