Tovuti za Vyama Vya Siasa nchini Tanzania
Baadhi ya vyama vya Siasa nchini Tanzania vimefungua tovuti zao ambazo huwawezesha watu mbalimbali kupata taaarifa na habari zinazohusiana chama, siasa na masuala mengine yanayoihusu nchi.
Wakati tunapoelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba, watu wengi walipo nje ya nchi pamoja na wafuatiliaji wa mambo wa Kimataifa wanapata taarifa nyingi kupitia kwenye mitandao, ambapo sehemu rasmi yakupata taarifa hizo ni kwenye tovuti rasmi za vyama na tume za uchaguzi.
Lakini ni jambo la kushangaza na kusikitisha sana, kwamba sehemu hii ya taarifa haijapewa kipaumbele kama vile redio, televisheni na magazeti. Baadhi ya tovuti za vyama hivi hazina habari mpya tangu zianzishwe. Nyingine zina taarifa zilizochapishwa muda muda mrefu sana il hali yamekuwepo matukio mengi ambayo yangestahili kuripotiwa tangu wakati huo hadi sasa.
Kwa kweli ni vigumu kung'amua ikiwa ni tatizo ni la kiteknolojia au tu kutokuipa kipaumbele TEKNOHAMA? Wahusika wa vyama na tovuti hizi tafadhalini kumbukeni kutumia tovuti zenu kupasha habari.
Zifuatazo ni orodha ya tovuti za baadhi ya vyama vya siasa nchini Tanzania. Tovuti za Tume ya Taifa ya uchaguzi pia zina tovuti ambazo anwani zake ni www.nec.go.tz na www.zec.go.tz
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA www.chadema.or.tz
Chama Cha Mapinduzi - CCM www.ccmtz.org
Civic United From - CUF www.cuf.or.tz
National Convention for Construction and Reform - NCCR-Mageuzi www.nccrmageuzi.or.tz
Ikiwa unafahamu anwani ya tovuti ambayo haijajumuishwa hapa, tafadhali tujuze katika kisanduku cha maoni na itaongezwa katika orodha hii kwa wepesi wa kuirejea na kuifikia.

Comments
Post a Comment