Sasa wateja wa CRDB na Vodacom M-PESA wanaweza kuweka na kutoa pesa
Wateja wa Vodacom M-PESA wenye akaunti katika benki ya CRDB sasa wanauwezo wa kuweka na kutoa fedha kutoka katika akaunti zao kupitia simu ya mkononi ya Vodacom iliyosajiliwa na huduma ya M-PESA. Kuzinduliwa kwa huduma hiyo sasa kunawapa urahisi zaidi wateja wa Vodacom M-PESA kuweka na kuchukua fedha zao kutoka akaunti ya benki kwa urahisi na unafuu zaidi mahali popote nchini na kwa wakati wowote pasi na kulazimika kufika katika tawi la benki ya CRDB.. Huduma hii ya ushirikiano kati ya Benki ya CRDB na kampuni ya Vodacom kupitia huduma yake ya M-PESA ni ya kwanza nchini na inalenga kuwaondolea usumbufu wateja wa M-PESA wa kupanga foleni ama kutembea umbali mrefu kufuata tawi la Benki. “Tunapoitambulisha huduma hii mpya inaamaanisha kwamba tumeongeza thamani nyengine katika simu ya mkononi na huduma ya Vodacom M-PESA.Mteja wa M-PESA kuweza kutoa na kuchukua fedha kutoka akaunti zao za CRDB kupitia simu zao za mkononi ni hatua nyengine muhimu ya kujivunia kuwa mteja wa