NAIBU WAZIRI MWANRI AIKATAA NYUMBA ILIYOKARABATIWA KIFISADI ,ASEMA LUDEWA SI SHAMBA LA BIBI

Ziara ya ghafla ya naibu waziri Mwanri kwenda kufichua ufisadi wa kutisha Lupanga kwa kukataa nyumba ya mganga iliyochakachuliwa ujenzi wake
Hii ni nyumba mpya ambayo bado inajengwa ila inavuja mabati yamechakaa kabla ya kuanza kutumika ipo Lupanga Ludewa ,naibu waziri hapa akitamani kutoa machozi kwa wizi huu wa kutisha
Hii ni nyumba mpya ambayo bado haijakamilika kujengwa ila imechoka mbaya haina tofauti na pagale Maajabu nyumba mpya ya mganga Lupanga Ludewa imechakaa kabla ya kuanza kutumika imekarabatiwa kwa Tsh,milioni 7 za serikali kupitia mradi wa Mamu
Hizi ndizo bati zenyewe zikiwa zinavuja kupitia kiasi,kweli Ludewa ni shamba la bibi
Kuta za nyumba hiyo kwa nje zikiwa zimepigwa lenda ila ndani lenda hakuna

NAIBU waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu anayeshughulika na serikali za mitaa na tawala za mikoa (TAMISEMI) Aggrey Mwanri amevunja ratiba iliyoandaliwa na viongozi wa wilaya ya kumtembeza katika miradi isiyo na matatizo na kuomba kupelekwa katika mradi wa ukarabati wa nyumba ya mganga wa zahanati Lupanga na kubaini ufisadi wa kutisha na kuagiza wilaya kusimamisha Mara moja ukarabati wa nyumba hiyo.

Naibu waziri huyo alifanya ziara hiyo leo katika wilaya ya Ludewa na kuonyesha kuwashangaza viongozi wa wilaya ya Ludewa baada ya kuivunja ratiba iliyopangwa na kuomba kupelekwa katika mradi huo ambao fedha zake kiasi cha shilingi milioni 7 zilizotengwa kukarabati nyumba hiyo kuonyesha kuchakachuliwa kutokana na mkandarasi kuezeka bati chakavu katika jengo hilo na kujengwa kuta kwa tope.

Akitoa maagizo kwa mkuu wa wilaya ya Ludewa Georgena Bundala baada ya kukagua ujenzi huo ambao mkandarasi wake Bw.Chanzy Mgaya kudai kuugua ghafla na kukimbizwa katika zahanati ya Mlangali katakana na kupata taarifa ya ugeni wa ghafla katika eneo lake la kazi .

Mwanri alisema kuwa amelazimika Kutembelea katika eneo hilou la ujenzi wa nyumba ya mganga bila ya kuwajulisha viongozi wa wilaya mapema baada ya kupokea taarifa za uchakachuaji wa kazi hiyo kutoka kwa wasamaria wema na taarifa kutoka katika ofisi za Tamisemi hivyo kulazimika kutoka eneo hilo.

Naibu waziri huyo alisema kuwa hatua ya kumwagiza mkuu huyo wa wilaya ya Ludewa na mkurugenzi kusimamisha Mara moja ujenzi huo ni baada ya kutorizishwa na kiwango cha ujenzi huo.

Alisema kasoro kubwa aliyoiona katika ujenzi huo ni jengo hilo kuja kubomoka kabla ya mganga husika kuanza kulitumia katakana na ujenzi wake kujengwa holela na kuwa mbaya zaidi nyumba hiyo inajengwa bila kuwekwa Lenda na kuwa mkandarasi huyo ameshindwa kujengwa nyumba kwa kiwango na kuwa hat a bati zinazotumika ni chakavu ambazo zimeanza kuvuja kabla ya nyumba kumalizika.

Hivyo alisema kuwa ni vema viongozi wa wilaya ya Ludewa wakachukia kwa yeye kusimamisha ujenzi wa nyumba hiyo ila fedha za umma zisitumike vibaya.

Kwa mujibu wa ratiba ya wilaya naibu waziri huyo alipaswa kapokelewa eneo la Lusitu majira ya saa 3.00 asubuhi ila naibu huyo alifika eneo hilo saa 2.23 asubuhi na kupokelewa na mbunge wa jimbo hilo la Ludewa Deo Filikunjombe na katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Ludewa Felix Haule ambao walikuwa katika msafara huo huku viongozi wa wilaya na madiwani wakifika eneo hilo na kumkuta naibu waziri huyo na msafara wake kutoka mkoani Iringa wakiwasubiri.

Pia ratiba ilikuwa ikionyesha kuwa baada ya naibu waziri huyo kukagua barabara ya Lusitu - Madilu na mradi wa umwagiliaji wa Mkiu msafara wake Ungeelekea Mlangali kukagua chumba cha upasuaji ila hakufanya hivyo aliomba msafara wake kuchepuka njiani Kwenda kijiji cha Lupanga kuona ukarabati wa nyumba hiyo ya mganga ambao katika ratiba haikuwepo.

Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Ludewa Monica Mchilo alimweleza naibu waziri huyo kuwa mkanadarasi huyo Mganya amekarabati nyumba hiyo kinyume na maagizo ya Baraza la madiwani na kuwa k kurudishia mabati chakavu katika nyumba hiyo.
,
Huku mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akimpongeza naibu waziri huyo kuwa kufanya ziara ya katika wilaya hiyo katika kipindi hike cha masika ambacho viongozi wengi wa kitaifa huwa hawafiki Ludewa. 


source http://francisgodwin.blogspot.com/

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA