Posts

HAPPY BIRTHDAY FRIDA

Image
Frida ni mmoja wapo wa wadau wakubwa wa blog hii,leo ni siku yake ya kuzaliwa. "Happy birthday, and may this day be a special one to always remember."

Maelezo ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kuhusu hoja za madaktari

Utangulizi Uongozi wa Wizara umekuwa ukifanya vikao mbalimbali na Viongozi wahusika wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) katika kutatua suala la Madaktari wanaofanya mazoezi kwa vitendo (internship) na hatimaye suala hili kumalizika. Baadaye MAT waliwasilisha Hoja nane za ziada Tarehe 21/01/2012. Wizara ilifanya mkutano na Uongozi wa Chama cha Madaktari kujadili hoja zilizowasilishwa. Wizara ilitoa maelezo kama ifuatavyo:- Madaktari kupewa nyumba za kuishi karibu na Hospitali Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na WIzara ya Fedha inarekebisha Waraka uliotolewa kwa Taasisi kuhusu ani anastahli kupewa nyumba, ili Madaktari waendelee kupatiwa nyumba bila kujali ngazi zao za mishahara. Pamoja na juhudi zinazofanywa na Mikoa na Halmashauri kuwapatia Nyumba Madaktari, Serikali imepata fedha kutoka Mfuko wa Dnia  (Global Fund) kwa ajili ya kujenga nyumba za Madaktari kwa kuanzia Wilaya 18 zilizo pembezo

HATA WEWE UNAWEZA KUSHIRIKI KWENYE HILI

Image
Taasisi ya Hassan Maajart Trust. Makusudi ya Taasisi hii ni kuhamasisha jamii kuchangia madawati na vifaa vingine katika shule zetu ili kufuta kabisa aibu ya watoto wa Kitanzania kukaa sakafuni wakiwa mashuleni. Taasisi hii pia ina duka la hisani yani 'Charity Shop' ambayo watu wanaleta nguo, viatu, vitabu, vyombo nk, vya zamani vyenye ubora na hali nzuri ambavyo hawafikiri kuvivaa tena, au kivitumia tena, na sisi tunaviuza second hand na hela zineanda kwenye mfuko wa madawati.

Miraba Minne ya Chipukizi

Image
Mwaka 2011 ulikuwa mzuri katika nyanja kadhaa za TZhiphop na miradi mingine , ingawa, kama kawaida,  changamoto za hapa na pale hazikosekani. Kwa upande wa wasanii, kwa ujumla wale chipukizi walioanza kusikika mwaka 2010 waliweza kujikita kwenye masikio na nyoyo za wengi. Mwamko wa mashabiki wanaoongezeka ni ushahidi thabiti. Kwa upande mwingine, tunapenda kuwaasa mashabiki pamoja na wasanii waendelee kujifunza kuhusu historia na misingi ya Hip Hop . Mwaka 2012 bila shaka unaonekana utakuwa mzuri zaidi. Wale waliochomoza mwaka 2010 na kufanya vizuri mwaka 2011 wanapevuka. Vivyo hivyo, wale walioanza kusikika mwaka 2011 wanaelekea kuzuri! Wasanii wanne chipukizi wanaojitegemea wameamua kuunganisha vichwa na kuunda Miraba Minne, chini ya uongozi wa mtayarishaji wa ala, Ray.  Ndani ya Miraba Minne kuna Maalim Nash (alikuwa anatumia jina ‘Nash MC’), P The MC , msanii mpya ndani ya M-Lab , Songa , na ZAiiD … Kaa tayari kupokea mixtape yao kwa mikono miwili . Tunatambul

Sasa wateja wa CRDB na Vodacom M-PESA wanaweza kuweka na kutoa pesa

Wateja wa Vodacom M-PESA wenye akaunti katika benki ya CRDB sasa wanauwezo wa kuweka na kutoa fedha kutoka katika akaunti zao kupitia simu ya mkononi ya Vodacom iliyosajiliwa na huduma ya M-PESA. Kuzinduliwa kwa huduma hiyo sasa kunawapa urahisi zaidi wateja wa Vodacom M-PESA kuweka na kuchukua fedha zao kutoka akaunti ya benki kwa urahisi na unafuu zaidi mahali popote nchini na kwa wakati wowote pasi na kulazimika kufika katika tawi la benki ya CRDB.. Huduma hii ya ushirikiano kati ya Benki ya CRDB na kampuni ya Vodacom kupitia huduma yake ya M-PESA ni ya kwanza nchini na inalenga kuwaondolea usumbufu wateja wa M-PESA wa kupanga foleni ama kutembea umbali mrefu kufuata tawi la Benki. “Tunapoitambulisha huduma hii mpya inaamaanisha kwamba tumeongeza thamani nyengine katika simu ya mkononi na huduma ya Vodacom M-PESA.Mteja wa M-PESA kuweza kutoa na kuchukua fedha kutoka akaunti zao za CRDB kupitia simu zao za mkononi ni hatua nyengine muhimu ya kujivunia kuwa mteja wa

HUYU NDIO BIBI ANAERAP NA KUIMBA

Image
Wakati nikisikiliza xxl leo huyu bibi kanivutia sana ukiangalia umri wake na nyimbo anazoimba hapo ndo utajua kuwa kama kipaji kipo basi kipo tuuuu na kamwe hakipotei picha na story hapo chini ni kutoka website ya www.millardayo.com huyu ndio bibi ambae ana rap na kuimba, maajabu yake ameyaonyesha kwenye XXL ya CLOUDS FM leo, stori kamili nitaiweka baadae kidogo hapa hapa millardayo.com na itasikika pia kwenye AMPLIFAYA. ana umri wa miaka 51, na mpaka sasa hajapata jina la kisanii la kutumia, track yake ya kwanza ameitoa leo kafanya na MH TEMBA

HAPPY BIRTHDAY RICHARD MFINANGA

Image
happy birthday my classmate Rich wish all da best in ur life and work hard so that u will reach to ur intended goals

LIGI KUU YA VODACOM KUANZA JUMAMOSI

Image
Bw.Boniface Wambura Ofisa HabariShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza keshokutwa (Januari 21 mwaka huu) kwa mechi nne. Moro United itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Mtibwa Sugar itaoneshana kazi na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani. Nayo Toto Africans itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani na Villa Squad itapambana na Kagera Sugar katika Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam. Januari 22 mwaka huu JKT Ruvu na Polisi Dodoma zitapepetana Uwanja wa Azam Chamazi wakati Januari 22 mwaka huu Dar es Salaam itakuwa na mechi mbili; African Lyon na Azam (Uwanja wa Azam Chamazi) na Simba na Coastal Union (Uwanja wa Taifa). Ratiba kwa ajili ya waamuzi na makamishna kwa mechi 35 za mwanzo tayari imeshatoka. Waamuzi wa kati 16 wameteuliwa kuchezesha mechi hizo huku watatu

AJIRA MPYA YA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI WENYE ELIMU YA SHAHADA MWAKA 2011/12

http://www.moe.go.tz/pdf/AJIRA%20MPYA%20YA%20WALIMU%20WA%20SEKONDARI%20-%20SHAHADA%202011-2012%20Final.pdf CLICK LINK HIYO HAPO JUU KUWEZA KUYATAZAMA.

NAIBU WAZIRI MWANRI AIKATAA NYUMBA ILIYOKARABATIWA KIFISADI ,ASEMA LUDEWA SI SHAMBA LA BIBI

Image
Ziara ya ghafla ya naibu waziri Mwanri kwenda kufichua ufisadi wa kutisha Lupanga kwa kukataa nyumba ya mganga iliyochakachuliwa ujenzi wake Hii ni nyumba mpya ambayo bado inajengwa ila inavuja mabati yamechakaa kabla ya kuanza kutumika ipo Lupanga Ludewa ,naibu waziri hapa akitamani kutoa machozi kwa wizi huu wa kutisha Hii ni nyumba mpya ambayo bado haijakamilika kujengwa ila imechoka mbaya haina tofauti na pagale Maajabu nyumba mpya ya mganga Lupanga Ludewa imechakaa kabla ya kuanza kutumika imekarabatiwa kwa Tsh,milioni 7 za serikali kupitia mradi wa Mamu Hizi ndizo bati zenyewe zikiwa zinavuja kupitia kiasi,kweli Ludewa ni shamba la bibi Kuta za nyumba hiyo kwa nje zikiwa zimepigwa lenda ila ndani lenda hakuna NAIBU waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu anayeshughulika na serikali za mitaa na tawala za mikoa (TAMISEMI) Aggrey Mwanri amevunja ratiba iliyoandaliwa na viongozi wa wilaya ya kumtembeza katika miradi isiyo na matatizo na ku

WALIMU WAFICHA WANAFUNZI KICHAKANI BAADA YA KUFUMWA NA NAIBU WAZIRI WAKITUMIKISHA WANAFUNZI

Image
Mwalimu wa shule ya msingi Luilo kata ya Lifua wilaya ya Ludewa mwalimu Mgaya akipita katika eneo ambalo wanafunzi walikuwa wakilima na kuacha majembe na kukimbia kujificha Msafara wa naibu waziri wa tamisemi Aggrey Mwanri ukipita eneo ambalo wanafunzi walikuwa wakilima Naibu waziri wa Tamisemi akiwahoji walimu na wanafunzi waliokuwa wakiwatumikisha watoto wa shule mida ya masomo leo Mwanafunzi wa shule ya Msingi Luilo Ludewa akiwa amebeba majembe baada ya naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri kuagiza warudi madarasani leo asubuhi Wanafunzi wa shule ya Msingi Luilo Ludewa wakiwa wamejificha katika kichaka pamoja na walimu wao kumkwepa naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri leo Wanafunzi wa shule ya msingi Luilo kata ya Lifua wilaya ya Ludewa wakilima shamba la shule mida ya masomo majira ya saa 3 asubuhi leo baada ya kufanya ziara ya ghafla eneo hilo BAADA ya naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Tamisem

FACEBOOK SONG BY DJ CLEO

Image
dj cleo - facebook .mp3 Found at bee mp3 search engine