Maelezo ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kuhusu hoja za madaktari
Utangulizi
Uongozi wa Wizara umekuwa ukifanya vikao mbalimbali na Viongozi
wahusika wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) katika kutatua suala la
Madaktari wanaofanya mazoezi kwa vitendo (internship) na hatimaye suala
hili kumalizika. Baadaye MAT waliwasilisha Hoja nane za ziada Tarehe
21/01/2012. Wizara ilifanya mkutano na Uongozi wa Chama cha Madaktari
kujadili hoja zilizowasilishwa. Wizara ilitoa maelezo kama ifuatavyo:-
Madaktari kupewa nyumba za kuishi karibu na Hospitali
Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais,
Menejiment ya Utumishi wa Umma na WIzara ya Fedha inarekebisha Waraka
uliotolewa kwa Taasisi kuhusu ani anastahli kupewa nyumba, ili Madaktari
waendelee kupatiwa nyumba bila kujali ngazi zao za mishahara.
Pamoja na juhudi zinazofanywa na Mikoa na Halmashauri kuwapatia
Nyumba Madaktari, Serikali imepata fedha kutoka Mfuko wa Dnia (Global
Fund) kwa ajili ya kujenga nyumba za Madaktari kwa kuanzia Wilaya 18
zilizo pembezoni zimechaguliwa kujengewa nyumba nane 98) kila Wilaya
kama sehemu ya kuboresha hali ya upatikanaji wa nyumba kwa Madaktari.
Kuongeza posho ya kuitwa kazini baada ya saa za kazi (on call allowance)
Wizara imefanyia kazi, maboresho ya pohso hiyo ya kuitwa kazini baada
ya saa za kazi (On call allowance), na imewasilisha kwa mamlaka husika,
kwa ajli ya kupata kibali. Mapendekezo hayo, yanatofautisha posho hiyo
kulingana na ngazi za Madaktari na watumishi wengine.
Rufaa za wagonjwa (hasa viongozi) wanaopelekwa kutibiwa nje ya nchi
Malalamiko ya Madktari ni kwamba baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wa
Serikali hushinikiza Daktari anayewahudumia awape rufaa ya kwenda
kutibiwa nje ya nchi hata kwa magonjwa yanayoweza kutibiwa hapa nchini.
Maelezo ya Wizara ni kwamba Wizara hugharamia matibabu nje ya nchi
kwa Watanzania wote bila kujali hali zao za kijamii au kisiasa ili mradi
vigezo vimetimizwa. Wizara hupokea rufaa za wagonjwa hao, ambazo
zimetokana na ushauri wa Jopo la Madaktari bingwa wa fani husika
wasiopungua watatu. Madaktari hao baada ya kuwachunguza wagonjwa na
kuamua kuwa wanahitaji rufaa huandika majina yao na fani zao katika fomu
za rufaa husika. Madaktari hao wana uhuru wa kuandika katika fomu ya
rufaa kama mgonjwa anastahili kupelekwa nje ya nchi au anaweza kutibiwa
hapa nchini na kwa hiyo hamna ulazima wa kumpelekea nje ya nchi.
Hata hivyo katika kipindi cha miezi mitatu (Oktoba hadi Desemba 2011)
jumla ya Wagonjwa 223 walienda nje kwa ajli ya matibabu, kati ya hao ni
awgonjwa 19 (8.5%) tu walikuwa viongozi wa Serikali na Siasa
(Waheshimiwa Wabunge na Viongozi waandamizi Serikalini).
Majina kwa ajili ya udhamini wa madaktari wanaochukua mafunzo ya Uzamili
Malalamiko ya Madaktari ni kwamba baadhi ya Madaktari waliopata
nafasi ya kuchukuwa mafunzo ya Uzamili katika Vyuo mbalimbali kukosa
udhamini wa Wizara.
Hapo awali ni Madaktari 50 tu kwa mwaka ndiyo walipata udhamini kwa
mafunzo ya Uzamili. Baada ya kuanza uktekelezaji wa Mpango wa Maendeleo
ya Afya ya Msingi (MMAM), hapo 2007, idadi hiyo iliongezeka na kufikia
Madaktari 300 kwa mwaka. Hii iliwezekana kutokana na Serikali kuwa na
fedha za kutosha kutokana na ufadhli wa Benki ya Dunia. Mwaka jana
ufadhili huu haukuwepo na hali ya fedha haikuwa nzuri, kiasi kwamba,
ilielekezwa kupunguza bajeti. Fedha iliyobaki ilitosha kudhamini
Madaktari 50 tu. Wizara inafanya jitihada za kutafuta fedha zkwa ajili
ya udhamini wa Madaktari waliokosa udhamini. Tayari baadhi ya Wadau wa
Maendeleo wako tayari kwa hili.
Kuhamisha Madaktari Bingwa wenye mikataba ya Ajira na Hospitali ya Taifa Muhimbili
Wizara kuwahamisha Madaktari Bingwa iliyoingia nao mkataba wa
udhamini wa masomo ya uzamili na wakati huo huo wakiwa na mikataba ya
ajira na Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wizra imekwisha rekebisha kasoro ya mikataba hiyo. Hospitali ya Taifa
Muhimbili tayari inatumia mikataba mipya inayoonesha kuwa daktari
akipata ufadhili wa Wizara atapangiwa kutuo kulingana na mahitaji ya
taifa.
Baada ya Serikali kupandisha hadhi ya hospitali za Mikoa kuwa
Hospitali za Rufaa na Mikoa, ni muhimu sana kwa Madaktari Bingwa kwenda
kufanya kazi katika hospitali hizo. Daktari Bingwa ndiye anayepaswa kuwa
kichocheo cha kuifanya Hospitali husika ipate rasilimali zinazotakiwa
(vifaa, watumishi, majengo na fedha). Aidha ataifanya hospitali hiyo
itoe huduma zinazotakiwa. Hii ni kulingana na Sera ya Afya na Mpango wa
Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMMAM). Mpango Mkakati wa Afya Na. 3
aunaozipandisha hadi Hospitali za Mikoa kuwa Rufaa, ili kuongoza huduma
za uningwa karibu na wananchi.
Posho ya mazingira hatarishi (Risk Allowance)
Hapo awali, Seirkali ilijumuisha posho mbalimbali kwenye mishahara ya
watumishi, piosho ya mazigira hatarishi ikiwa ni mojawapo ya posho
hizo. Hata hivyo, Serikali imetambua umuhimu wa kuzitenganisha posho
hizo na mishahara kwa watumishi wa kada za afya wanaofanya kazi katika
mazingira hatarishi. Wizara kwa kushirikiana na mamlaka husika
wanalifanyia kazi suala hili.
Ajira za Madaktari
Wizara imewaajiri Madaktari wote walioomba kuajiriwa. Tatizo kubwa ni
kwamba wengi wa Madaktari hao hawaendi kule wanakopangiwa kwa kuwa
wanapenda kbaki Dar es Salaam, ambapo hata hivyo nafasi ni chache.
Ilikubalika kuwa MAT na vyama vingine vya kitaaluma viwe ni wadau katika
kutoa taarifa kwa Madaktari na Wataalamu wengine kuhusu kuwepo kwa
nafasi za ajira za Madaktari.
Aidha Serikali imekuwa ikiongeza nafasi za ajira za watumishi wa kada
za Afya kutoka nafasi 1,677 mwaka 2005/2008 hadi kufikia nafasi 9.391
kwa mwaka wa fedha 2011/2012.
Kutaka Mshahara wa Shilingi Milioni 3.5 kwa mwezi
Mishahara ya watumishi wa Serikali, hufuata Miundo ya Utumishi
(Scheme of Service) iliyopo. Aisha, serikali imeboresha muundo wa
watumishi wa sekta ya afya. Baada ya kuboreshwa kwa muundo huo, kwa hivi
sasa, Watumishi wa afya wanapata mishahara mikubwa kuliko watumishi
wengine serikalini.
Wito kwa Madkatari walio katika mgomo
Wakati serikali inashughulikiwa hoja za Madaktari, Wizara inatoa wito
kwa Madkatari wote kurudi na kuendelea kufanya kazi za utabibu ili
kuokoa maisha ya Watanzania, kama tulivyokubalina katika kikao na
viongozi waliokuja Wizarani tarehe 21/01/2012.
Ni vyema Madaktari wakatambua juhudi zinazofanywa na serikali, za
kuboresha maslahi ya watumishi wa sekta ya afya, kama ilivyoelezwa hapo
juu, na kuziunga mkono.
Hata hivyo, serikali inatamka kuwa, milango iko wazi ya kujadili masula ahaya, na wataalamu wote wa sekta ya afya.
Asanteni kwa kunisikiliza
Imetolewa: 26/01/2012
Comments
Post a Comment