Posts

TWANGA PEPETA KUWAPA BURUDANI WAKAZI WA MUSOMA

Image
Bendi ya Muziki wa Dansi ya Twanga Pepeta imepania kukonga nyoyo za wapenzi wa bendi hiyo na wapenzi wote wa Muziki Mjini Musoma siku ya Ijumaa ya Machi 31 pale watakapofanya onyesho lao la kwanza Mjini hapa baada ya kufanya hivyo takribani miaka 3 iliyopita. Akizungumza na mwakilishi wa blog hii kutoka Musoma Bwana Shomari Binda kwa njia ya simu wakiwa njiani kuja Musoma,mratibu wa ziara hiyo ambayo ni maalumu kwa wakazi wa Kanda ya ziwa Martin Sospeter amesema kuwa wamefanya maandalizi ya kutosha kwa muda wote ili kuhakikisha wanatoa burudani ambayo itakidhi haja kwa wale wote watakaobahatika kufika kuangalia onyesho la bendi hiyo. Amesema katika ziara hiyo wataitambulisha Album yao mpya inayokwenda kwa jina la Dunia Daraja ambapo ndani yake kuna nyimbo kama vile Mapenzi hayana kiapo,Penzi la Shemeji,Mtoto wa Mwisho pamoja na nyi ngine zilizomo katika Album hiyo. Martini amesema kuwa licha ya kupata Burudani ya nyimbo mpya za Bendi hiyo,wapenzi wa Twanga Pepet

HUDUMA MPYA YA KISASA INAYOKUUNGANISHA MTANDAO WA MICHUZI BLOG BURE

Image
Tovuti yako uipendayo inakupa huduma ya kujivinjari bure kutoka Uhuruone Muhidini Issa Michuzi akishikiriana na Uhuruone wanawapatia wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya “Wifi hotspots” ambayo itawapa wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya bure ya kutembelea tovuti ya Michuzi. Kwa kupitia mitambo yao ya “Wifi Mesh” iliyopo Dar es Salaam ambayo imeunganishwa na tovuti ya Michuzi,wakazi wa Dar es Salaam wanatangaziwa kwamba wawashe kompyuta zao na kuunganishwa na taarifa za punde bila gharama yoyote. Akikaririwa katika mahojiano ndugu Issa Michuzi alisema hivi, “Ni mapinduzi ya kweli ambapo Watanzania wanachukua hatua katika kuleta taarifa mbalimbali kwa wananchi katika viwango nafuu. Ninaamini hii itaongeza mawasiliano kwa watu wetu na ni ndoto yangu kwamba tovuti ya Michuzi itakua huru kufika kwa Watanzania wote hivi karibuni”. Akiwa ofisini Bwana Rajabu Katunda alisema, “Uhuruone imejikita katika kutoa huduma kwa jamii na tumegundua

WABUNIFU WA MAVAZI NA WANAMITINDO KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE ONYESHO LA 'SOUTH AFRICA FASHION WEEK'

Image
Millen Magese (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanamitindo na wabunifu watakaokwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki katika maonyesho ya 'South Africa Fashion Week ' WABUNIFUwatatu, Doreen Estazia Noni anayetumia Lebo ya eskado bird , Jamila Vera Swai na Evelyne Rugemalira wamepata nafasi ya kuchaguliwa kwenda kwenye maonyesho ya mitindo yajulikanayo kama South Africa Fashion Week nchini Afrika kusini kupitia kampuni ya Millen Magese Group company Limited. Wabunifu hao watapanda jukwaani siku ya Aprili Mosi katika onyesho linalobeba jina la Tanzania International Fashion Exposé (TIFEX) by Millen Magese introducing Eskado Bird, Jamila Vera Swai and Evelyne Rugemalira. Millen alipata fursa ya kutembelea wabunifu hao na kujionea jinsi walivyokuwa wabunifu katika fani hiyo na kuhamasika kuwachukua na kushiriki katika maonyesho hayo maarufu ya mitindo katika bara la Afrika. Alisema kuwa amevutiwa sana na jinsi walivyokuwa

MANISPAA YA MUSOMA YAANDAA MIKAKATI YA KUBORESHA USAFI

Na Shomari Binda, Musoma Halimashauri ya Manispaa ya Musoma Mkoani Mara imeandaa mikakatia mbalimbali ya kuhakikisha Manispaa hiyo inakuwa katika hali ya usafi na kuwa miongoni mwa Miji misafi hapa Nchini kama ilivyokuwa katika Miaka ya nyuma. Kauli hiyo imetolewa jana na Afisa wa Afya wa Manispaa ya Musoma Peter Mtaki Ofisini kwake alipokuwa akizungumza na BINDA NEWS kuhusiana na maandalizi ya uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa mazingira itakayoanza Machi 30. Alisema moja ya mikakati ambayo wameipa kipaumbele ni pamoja na kusimamia Sheria ndogo ndogo za usafi wa Mazingira zilizotungwa mwaka 2010 ambazo bado zinaendelea kutumika hadi sasa lakini zimekuwa hazizingatiwi na Wananchi. Mtaki alidai Sheria hizo zinamtaka kila mkazi kuweka eneo lake safi kuanzia majumbani,eneo lake la kazi na maeneo ya Biashara pamoja na kuchangia gharama za Usafi kama ada ya Usafi. Alieleza kuwa Sheria hiyo inatamka kwa wale wanaokuwa wagumu wa kutojali usafi na ku

SIMBA KUJICHIMBIA MISRI KUNOA MAKALI YA ES SETIF

Image
KATIKA kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa marudiano wa kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya ES Setif ya Algeria wiki ijayo, kikosi cha Simba kimepanga kwenda kuweka kambi nchini Misri siku tano  kabla kuelekea Algeria katika mchezo wa marudiano. Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema kuwa wanalazima kwenda mapema huko ili kuweza kuzoea hali ya hewa ya huko kwani kwa sasa Algeri kuna baridi kali hivyo kwa kuwa Misri haitofautiani sana itakuwa ni vizuri kwa kikosi chao. Alisema  kikosi chake kinaendelea na mazoezi ya kawaida kujiandaa na michezo yake ya Ligi kuu soka Tanzania Bara. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jumapili, Simba iliwabanjua waarabu hao mabao  2-0, huku mechi ya marudiano ikitaraji kupigwa  ugenini kati ya Aprili 5-8 mwaka huu.

NIMPENDE NANI YA DIAMOND KUONEKANA VIDEONI

Image
MSANII wa muziki wa kizazi bongo Nassib Abdul ‘Diamond’ , amesema kuwa April 20 mwaka huu, itakuwa ni siku maalum kwake kwani atakuwa anaitambulisha video ya wimbo wake wa ‘Nimpende Nani’. Wimbo huo umefanya vizuri na kuwa gumzo kubwa ndani ya jamii kwani baadhi ya mashabiki wake walihisi ngoma hiyo ni swali kwao ili wampe jibu kati ya Wema Sepetu na Jokate, ampende nani lakini haupo katika mtazamo huo. Msanii huyo alisema kuwa kufanya vizuri kwa wimbo huo ndiko kuliko mpa hamasa ya kutoa video yake kwani anaamini hata hiyo itafanya vizuri. “April 20 mwaka huo video yangu itakuwa sokoni hivyo nawaomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwani siku si nyingi wataona ukweli wote unaopatikana ndani ya wimbo huo,” alisema. Hata hivyo msanii huyo wa nyimbo ‘Mbagala’ , aliongeza kuwa Ijumaa ya wiki hii atakuwa na shoo kubwa kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Lengo kubwa la kufanya shoo hiyo ni kuwakutanisha watu hasa vio

KATIKA PICHA UTENGENEZAJI WA VIDEO YA SINGLE BOY YA ALLY KIBA & LADY JAYDEE

Image
  Hizi ni baadhi ya picha zilizochukuliwa wakati wa utengenezaji wa video hiyo,so stay tune  picha ni kwa hisani ya www.millardayo.com