Posts

JK AONGOZA WATANZANIA KATIKA SHEREHE ZA MUUNGANO JIJINI DAR LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wananchi wakati alipokuwa akiingia katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuongoza maadhimisho ya mika 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo asubuhi. Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba wakati alipowasili katika uwanja wa Uhuru kuongoza sherehe za Muungano zilizofanyika leo jijini Dar es salaam

HOW TO DEVELOP IDEAS

1. Be a good observer. Keep your eyes and ears open to what is going on around you. 2. Let your mind play with ideas. Play with ideas by letting them bounce around in your mind in a nonsensical way. 3. Don't be critical during ideation. Be sure not to discard any ideas too soon. 4. Piggyback off others. Listen to the people around you and use their ideas to stimulate ideas of your own. 5. Be fluent. Remember that the more ideas you generate, the more probable it is that one of them will be a good idea. 6. Be open-minded. Don't allow narrow thinking to stop the development of your ideas. 7. Daydream. Set aside time during the day to exercise your imagination by daydreaming. 8. Know when to relax. When ideas are stale, get away from them by relaxing via tennis, biking, reading, etc. 9. Keep a notebook of ideas. Be sure to keep a small notebook handy at all times in which to record ideas so th

Leo ni siku ya kumbukumbu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Mwalimu wa Historia skuli alinifunza kuwa ni ziliunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili 1964. Unaweza kujipakulia nakala zifuatazo ili kuongeza maarifa kuhusu historia na mambo ya Muungano huu: INTELLIGENCE  STUDY ZANZIBAR:  T H E   HUNDRED  DAYS' REVOLUTION (ESAU  XXX) DIRECTORATE  OF INTELLIGENCE -  foia.cia.gov/CPE/ESAU/esau-28.pdf The Union between Tanganyika and Zanzibar  LEGALITY OF ADDITIONAL MATTERS OUTSIDETHE ARTICLES OF UNIONBY MUSSA, ALI. UBWA -  zanzinet.org/files/legality_union.pdf KWAHERI UKOLONI, KWAHERI UHURU! ZANZIBAR NA MAPINZUZI YA AFRABIA :  Dkt. Harith Ghassany -  kwaherikwaheri.com/download.htm Mohamed Said anjibu vipi "East African Muslim Welfare Society" ilivunjwa -  youtube.com/user/MzeeBarwani Baadhi ya maoni ya watu na vikundi kuhusu Muungano -  Muungano in site:mzalendo.net

Ofisi Ya Katibu UVCCM Arusha Yafungwa

Image
HALI ya Siasa Mkoa wa arusha hususan kwa Umoja wa Vijana (UVCCM) ni tete baada ya vijana hao  kuchukua uamuzi wa kufunga ofisi ya umoja huo pamoja na kubandika mabango usiku wa kumkia leo . Mabango hayo yalikuwa yakimshinikiza Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Abdallah Mpokwa kuondoka na kumfuata aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM ,James Ole Millya ambaye amehamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na mengine yakimtuhumu Millya kuwa ni fisadi . Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya vijana wa umoja huo mkoani hapa ambao ni Ally Shabani maarufu kwa jina la Majeshi ambaye ni Katibu wa UVCCM Kata ya Moivo  pamoja na Masoud Rajabu ambaye ni Katibu wa UVCCM kata ya Lemara walisema wamechukizwa na kauli ya Mpokwa aliyoitoa janajuu ya kumsafisha Millya kwa madai hana ushahidi wa hela Sh. milioni 2 iliyotolewa kwa ajili ya  kuanzishwa kwa saccos hiyo. Shabani alisema kauli aliyoitoa  juzi Mpokwa kuwa  UVCCM haijawahi kuwa na mradi wa SACCOS na pia kukanusha suala la Millya kut

WATU WANNE (4) WAUWAWA KIKATILI ARUSHA.

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kushoto) akiongea muda mfupi baada ya kuangalia miili ya watu wanne waliouawa kinyama na kutupwa maeneo tofauti. Wapi kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye akiwa na maofisa usalama katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hospital ya Mkoa, Mount Meru jana   Maiti wakiwa wamelundikwa kwenye gari la polisi baada ya kugundulika wametupwa maeneo mbalimbali wilayani Arumeru jana. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kushoto) akiangalia miili ya watu wanne waliouawa kinyama na kutupwa maeneo tofauti. Wapi kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye akiwa na maofisa usalama katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hospital ya Mkoa, Mount Meru jana. Picha na Mdau Richard Mwaikenda   NAOMBA RADHI KWA KUZIONYESHA PICHA HIZI

KIFO CHA ZAOLA PARETO TANZANIA

Image
Zao la pareto ni miongoni mwa mazao ambayo wakulima wamekuwa wakipunguza na kuacha kuyalima kabisa, huenda ni kutokana na bei yake kuwa chini au soko sumbufu. Kamera ya Benjamin Kaminyonge ilipita maeneo ya wilaya ya Makete, kata ya Matamba na kuona zao hilo likiwa kwenye shamba la ekari moja ndani ya kijiji kizima huku kukiwa na mazao kama mahindi, ngano, maharage na alzeti kwa wingi. (picha: benjaminkaminyoge.blogspot.com)

VIJANA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA MAKUNDI HATARISHI

Vijana Mkoani Mara wametakiwa kutojihusisha na makundi korofi na hatarishi na badala yake kujiunga na Club za Vijana ambazo zina lengo la kuleta mabadiliko na kupeana mawazo ambayo yatawasaidia katika maisha katika kujiendeleza na kupata mafanikio ya Kiuchumi,Elimu na mambo mengine ya msingi. Kauli hiyo imetolewa na Mratibu msaidizi wa Idara ya Vijana ya Youth to Youth kutoka Jijijini Mwanza Sadick Bakary alipokuwa akizungumza na mwakilishi wa blog hii kutoka Musoma Bw. Binda kuhusiana na kampeni ya kuhamasisha Vijana Mkoani Mara kuepukana na kujiiingiza katika makundi hatarishi ambayo yamekuwa hayana faida na kuanzisha Club ambazo zitawasaidia kuwa na mtazamo wa mabadiliko ya kimaisha. Alisema kijana kama kijana anaweza kutatua tatizo la kijana mwenzake kwa kumpa mawazo na kusikilizwa hivyo kwa kuanzisha Club kama hizo za vijana kutaweza kupata nafasi ya kukutana na kuweza kupeana mawazo ya kubadilika na kuwa na mawazo ya kujishughulisha kwa kutafuta kipato halali n