VIJANA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA MAKUNDI HATARISHI
- Get link
- X
- Other Apps
Vijana Mkoani Mara wametakiwa kutojihusisha na makundi korofi na
hatarishi na badala yake kujiunga na Club za Vijana ambazo zina lengo la
kuleta mabadiliko na kupeana mawazo ambayo yatawasaidia katika maisha
katika kujiendeleza na kupata mafanikio ya Kiuchumi,Elimu na mambo
mengine ya msingi.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu msaidizi wa
Idara ya Vijana ya Youth to Youth kutoka Jijijini Mwanza Sadick Bakary
alipokuwa akizungumza na mwakilishi wa blog hii kutoka Musoma Bw. Binda kuhusiana na kampeni ya kuhamasisha
Vijana Mkoani Mara kuepukana na kujiiingiza katika makundi hatarishi
ambayo yamekuwa hayana faida na kuanzisha Club ambazo zitawasaidia kuwa
na mtazamo wa mabadiliko ya kimaisha.
Alisema kijana kama
kijana anaweza kutatua tatizo la kijana mwenzake kwa kumpa mawazo na
kusikilizwa hivyo kwa kuanzisha Club kama hizo za vijana kutaweza kupata
nafasi ya kukutana na kuweza kupeana mawazo ya kubadilika na kuwa na
mawazo ya kujishughulisha kwa kutafuta kipato halali na kuweza kupeana
Elimu zaidi ya kujiendeleza.
Alidai Club hizo zitasaidia
kumfanya kijana kujitambua na kuona tatizo la kijana mwenzake kama
tatizo lake na kuweza kumsaidia ili mwenzake aweze kuonekana kijana
ambaye hana matatizo na kuweza kupata fursa za kupata msaada kutoka
katika jamii na watu wanaomzunguka katika shughuli za kila siku.
"Vijana ambao watakuwa katika Club hizi zitakazoanzishwa atakuwa na
mawazo ya kuwatoa vijana katika makundi hatarishi na kumpa halisi ya
matendo hasa juu ya ukatili wa aina yeyote kwa Wanawake,Wasichana na
Watoto kwa kuwa vijana wanayo nafasi kubwa na kufanya kazi hiyo.
"Tunataraji kuanziasha Club hizi Mashuleni na Mitaani na kuhamasisha
vijana kujiunga kwa wingi ili kwa namna moja ama nyingine tuweze
kubadilishana mawazo na kuweza kukomesha vitendo vya ukorofi ambavyo
havina tija na kuwa kitu kimoja katika kuleta mabadiliko ya
kimaisha,"alisema Sadick.
Alisema kwa upande wa Mkoani Mwanza
mpaka sasa kumeanzishwa Club 180 ambazo zimeungana na kuunda Muungano wa
Vijana Mkoa wa Mwanza na wanafanya kazi ya kuhamasisha Vijana
kutojiunga na makundi hatarishi na kukomesha masuala yote ya unyanyasaji
na kufanya shughuli za kujipatia kipato kwa kupitia Elimu ya
ujasiriamali ambayo wamekuwa wakiipata kupitia Club zao
Aliongeza kusema kuwa mpaka sasa wamekwisha tembelea Club 13 katika Mkoa
wa Mara na wataendelea kuhamasisha ili lengo la kuwakusanya Vijana na
kuzungumza nao kuhusiana na athari ambazo zinapatikana katika kujiingiza
katika makundi hatarishi.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment