JUA CALI AFUNIKA USIKU WA BORNFIRE CHUO CHA SAUT
Usiku wa kuamkia leo Msanii BABA YAO..... JUA CALI aka MGENGE kutoka pande za NAII-Kenya amewarusha maelfu ya wanafunzi wa SAUT pamoja na wananchi wanaokizunguka chuo hiki waliojitokeza katika viwanja vya Raila Odinga katika lile tamasha linalojulikana kama Bornfire, kwa ajili ya kuwakaribisha wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza na wale wanafunzi wa Masters. Msanii JUA CALI alipanda jukwaani muda wa saa 12:56 usiku huku mashabiki wake wakiwa wanamsubilia kwa hamu kubwa,japokuwa tamasha hili liliambatana na manyunyu ya mvua hapa na pale lakini mashabiki wake hawakukata tamaaa. Jua kali aliwapangaisha mashabiki wake kwa muda kama wa dakika 35 huku watu bado wakiwa na hamu kubwa ya kuendelea kumsikiliza, vibao vikali kama "Kwaheri","Bidii","Ngeli ya genge" "manzi amejibeba","Niimbie"aliyoimba na mwanadada Enika viliwakuna sana mashabiki wake huku DJ wake akionyesha ufundi wa kucheza na turntable. moto huu ndo unawakili