Posts

SEMINA YA UJASIRIAMALI YA BURE-TANDALE KUANZA APRILI 1-4, 2015

Image

ZITTO KABWE ACHAGULIWA KUWA MKUU WA CHAMA CHA ACT TANZANIA

Image
Kiongozi mpya wa chama cha ACT Tanzania, Zitto Kabwe akionyesha alama ya chama ambayo ni "Uwazi" baada ya kuchaguliwa.      Zitto akihutubia wajumbe.                 Zitto akihutubia wajumbe wakati wa uchaguzi huo. (P.T)                 Wajumbe wakiserebuka wakati wa uchaguzi huo.        Wajumbe wakifurahi kwa kushikana mikono kuonyesha umoja.    Wajumbe wakipiga kura. Zitto Kabwe, akilakiwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho, wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika kwenye ukumbi wa Kadinali Rugambwa, Oysterbay jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 28, 2015. Zitto alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama hicho nafasi ambayo kwa katiba ya chama hicho ndiyo ya juu zaidi. Nafasi zingine ni Mwenyekiti wa chama, na makamu wake, wa Tanzania visiwani na Tanzania bara, hali kadhalika nafasi ya ukatibu mkuu na manaibu wake wiwili.  Mama Anna Mughwira kawa Mwenyekiti wa kwanza wa chama cha ACT Wazalendo na kuweka rekodi nchini Tanzania. Mwenyekiti wa Tai

MATOKEO YA UCHAGUZI NIGERIA LEO JIONI

Image
Matokeo ya uchaguzi Nigeria leo jioni Mama akipiga kura nchini Nigeria Wasimamizi wa uchaguzi wakiwahakikika wapiga kura kabla ya kupiga kura zao. Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni. Upigaji kura uliendelea katika siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura. Mama akipiga kura nchini NigeriaKauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, INEC, Attahiru Jega. "Tumaini letu na ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi kwa bidii ni kuweza kutangaza matokeo ya uchaguzi ndani ya saa arobaini na nane na tunatumaini muda mchache zaidi kuliko ule wa mwaka 2011. Imeanza kutoka saa 48 baada ya uchaguzi kumalizika jana. Kwa hiyo tumeanza kuhesabu saa arobaini na nane kwa kweli kutoka jana jioni wakati idadi ya kutosha ya majimbo yalipofanya uchaguzi." Bwana Jega amesema

Nusura Watu Wagongwe Na Magari Baada Ya Davido Kurusha Kibunda Cha Mkwanja Katikati Ya Barabara

Image
Msanii ambae ameshakuja Tanzania mara mbili, mkali kutoka Nigeria Davido hivi karibuni alirusha kibunda cha pesa katikati ya barabara ilibaki kidogo watu wagongwe na magari kwa kuzikimbilia pesa hizo  Mara nyingi unashauriwa kama unaona unapesa nyingi hadi nyingine unaona hazina kazi, nenda katoe misaada kwa watoto yatima, toa misaada katika makanisa na misikiti.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU, MACHI 30 YAPO HAPA

Image
Na Awadh Ibrahim

WAFUNGWA NCHINI KENYA KUTOPATA CHAKULA CHA BURE WAKATI WA KUTUMIKIA VIFUNGO VYAO

Image
Sheria mpya nchini kenya kuanza kutumika kwa wafungwa wote wanaotumikia vifungo vyao kutopata chakula cha bure magerezani, hayo yamesemwa na  waziri wa usalama Joseph Nkaissery wa  nchini  kenya kwamba wafungwa hao wanatakiwa kuisaidia serikali katika kushiriki kwenye maswala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara  ili kupunguza gharama kubwa ambayo serikali inatumia kwa ajili ya kuwatunza. Nkaissery anasema kwamba inakuwaje serikali itumie pesa nyingi kuwalisha watu waliovunja sheria na kuishia kufungwa, hivyo wanapaswa kuwa sehemu ya kuleta maendeleo ya Taifa na sio kuwahifadhi watu wanao liingiza taifa katika hasara. Nyanja Kelvin Poti Like  ·  Comment  ·  Share  ·  603 804 88

Faini zilizopigwa na TFF kwa timu, wachezaji

Kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kilichoketi jumanne ya tarehe 24, Machi 2015 jijini Dar es salaam, kimepitia taarifa mbalimbali za michezo iliyochezwa na kutoa adhabu kwa wachezaji na vilabu vya Ligi Kuu ya Vodacom. Katika mechi namba 107 iliyowakutanisha wenyeji Ndanda FC dhidi ya Coastal Unioni, klabu ya Ndanda imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu ya Vodacom kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi Anold Bugado. Mechi namba 108 iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, (Stand United dhidi Simba SC), wenyeji timu ya Stand United imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(8) kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika ishirini. Mchezo namba 117 uliozikutanisha Simba SC dhidi ya Yanga SC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, timu ya Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14

MADA MAUGO AMCHAKAZA KASEBA KWA KO

Image
Bondia Mada Maugo amemaliza ubishi kwa kumtwanga Japhet Kaseba kwa KO. Maugo amemchapa Kaseba katika raundi ya nane katika pambano lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar. Pambano hilo lilikuwa la kumaliza ubishi kati yao na Maugo alitawala raundi mbili za mwanzo, kabla ya Kaseba kutawala raundi ya tatu na nne. Kaseba alishindwa kuvumilia mapigo ya Maugo baada ya kuchapwa kwa konde kali la kushoto na kuanguka katika raundi ya nane. Juhudi zake za kuinuka zilishindikana na kumpa ruhusa mwamuzi kumaliza pambano hilo. Katika pambano jingine, Karama Nyilawila naye alimshinda Ibrahim Tambwe kwa KO katika raundi ya pili. Na Ashraf naye akammaliza Ally Ramadhani kwa TKO katika raundi ya pili tu.(CHANZO:GPL) (Daniel kilonge)

AUSTRALIA: KUNA UWEZEKANO WA KENYA KUSHAMBULIWA

Image
Serikali ya Australia imetahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea mashambulizi ya kigaidi kwenye maeneo yenye watu wengi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi ingawa indhari hiyo haikutaja ni lini au ni makundi yapi yanayopanga kutekeleza mashambulizi hayo. Taarifa ya serikali ya Australia imewataka raia wake kuwa makini wanapoitembelea Kenya hususan jiji la Nairobi. Ingawa serikali ya Kenya haijatoa radiamali yoyote kuhusu indhari hiyo ya Australia, katika siku za huko nyuma Kenya imekuwa ikikosoa taarifa kama hizo ikisema zinaathiri sekta ya utalii lakini pia zinawapa magaidi fursa ya kujipiga kifua na kuwa na hamasa zaidi. Siku chache zilizopita, Marekani ilitoa indhari kama hiyo dhidi ya mji wa Kampala huko Uganda na kusema taarifa za kiintelijensia zinaonyesha kuwa magaidi wanapanga kushambulia maeneo yenye kutembelewa zaidi na raia wa kigeni mjini humo. (CHANZO: IDHAA YA KISWAHILI TEHRAN) 

WANIGERIA WAPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS

Image
Taifa lenye wakaazi wengi barani Afrika, Nigeria, linapiga kura Jumamosi(28.03.2015)kumchagua rais mpya, katika uchaguzi ambao una mvutano mkubwa kuwahi kuonekana tangu nchi hiyo kupata uhuru. Wagombea wakuu katika uchaguzi wa Nigeria,  Mohammadu Buhari  na  Goodluck Jonathan (kulia) Kuanzia mji mkubwa kabisa wa Lagos katika eneo la Wakristo upande wa kusini mwa nchi hiyo hadi katika miji upande wa kaskazini ambako kunapatikana Waislamu wengi, vituo vya kupigia kura vilitarajiwa kufunguliwa mapema asubuhi, ambapo kiasi ya Wanigeria milioni 68.8 kati ya wakaazi milioni 173 wamejiandikisha kupiga kura. Rais Goodluck Jonathan amewasili kwa helikopta katika mji alikozaliwa wa Utuoke kusini mwa jimbo la Bayelsa usiku wa jana Ijumaa, kwa matumaini ya kupata muhula wa pili wa uongozi licha ya ukosoaji mkubwa katika rekodi yake. Mpizani wake mkubwa , mtu aliyejitangaza kupambana na ufisadi katika serikali Muhammadu Buhari , alikuwa mjini Daura, katika jimbo la kaskazini la Kat

KIBONZO CHA LEO JUMAMOSI

Image
Imechotwa kutoka kwenye mtandao wa kijamii.

MAPITIO YA MAGAZETI YAKISOMWA KATIKA TV MBALIMBALI MACHI 27, 2015

Image
Mapitio ya magazeti katika Tv mbalimbali Machi 27, 2015