WANIGERIA WAPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS


Taifa lenye wakaazi wengi barani Afrika, Nigeria, linapiga kura Jumamosi(28.03.2015)kumchagua rais mpya, katika uchaguzi ambao una mvutano mkubwa kuwahi kuonekana tangu nchi hiyo kupata uhuru.
Nigeria - nominierter Präsidentschaftskandidat Muhammadu Buhari und Goodluck Jonathan
Wagombea wakuu katika uchaguzi wa Nigeria, Mohammadu Buhari na Goodluck Jonathan(kulia)
Kuanzia mji mkubwa kabisa wa Lagos katika eneo la Wakristo upande wa kusini mwa nchi hiyo hadi katika miji upande wa kaskazini ambako kunapatikana Waislamu wengi, vituo vya kupigia kura vilitarajiwa kufunguliwa mapema asubuhi, ambapo kiasi ya Wanigeria milioni 68.8 kati ya wakaazi milioni 173 wamejiandikisha kupiga kura.
Rais Goodluck Jonathan amewasili kwa helikopta katika mji alikozaliwa wa Utuoke kusini mwa jimbo la Bayelsa usiku wa jana Ijumaa, kwa matumaini ya kupata muhula wa pili wa uongozi licha ya ukosoaji mkubwa katika rekodi yake.
Mpizani wake mkubwa , mtu aliyejitangaza kupambana na ufisadi katika serikali Muhammadu Buhari , alikuwa mjini Daura, katika jimbo la kaskazini la Katsina, akilenga kurejea kwa njia ya kidemokrasia madarakani baada ya kuwapo madarakani kwa muda kama mtawala wa kijeshi katika miaka ya 1980.(Daniel kilonge)

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA