AUSTRALIA: KUNA UWEZEKANO WA KENYA KUSHAMBULIWA


Serikali ya Australia imetahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea mashambulizi ya kigaidi kwenye maeneo yenye watu wengi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi ingawa indhari hiyo haikutaja ni lini au ni makundi yapi yanayopanga kutekeleza mashambulizi hayo. Taarifa ya serikali ya Australia imewataka raia wake kuwa makini wanapoitembelea Kenya hususan jiji la Nairobi. Ingawa serikali ya Kenya haijatoa radiamali yoyote kuhusu indhari hiyo ya Australia, katika siku za huko nyuma Kenya imekuwa ikikosoa taarifa kama hizo ikisema zinaathiri sekta ya utalii lakini pia zinawapa magaidi fursa ya kujipiga kifua na kuwa na hamasa zaidi.

Siku chache zilizopita, Marekani ilitoa indhari kama hiyo dhidi ya mji wa Kampala huko Uganda na kusema taarifa za kiintelijensia zinaonyesha kuwa magaidi wanapanga kushambulia maeneo yenye kutembelewa zaidi na raia wa kigeni mjini humo.
(CHANZO: IDHAA YA KISWAHILI TEHRAN) 

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA