MATOKEO YA UCHAGUZI NIGERIA LEO JIONI

Matokeo ya uchaguzi Nigeria leo jioni
Mama akipiga kura nchini Nigeria
Wasimamizi wa uchaguzi wakiwahakikika wapiga kura kabla ya kupiga kura zao.
Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni.

Upigaji kura uliendelea katika siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura.

Mama akipiga kura nchini NigeriaKauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, INEC, Attahiru Jega. "Tumaini letu na ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi kwa bidii ni kuweza kutangaza matokeo ya uchaguzi ndani ya saa arobaini na nane na tunatumaini muda mchache zaidi kuliko ule wa mwaka 2011. Imeanza kutoka saa 48 baada ya uchaguzi kumalizika jana. Kwa hiyo tumeanza kuhesabu saa arobaini na nane kwa kweli kutoka jana jioni wakati idadi ya kutosha ya majimbo yalipofanya uchaguzi."
Bwana Jega amesema alitumaini jumuia ya kimataifa inaweza kupongeza namna Nigeria ilivyoendesha uchaguzi."Tunaamini tumefanya vizuri kabisa. Hatuwezi kupuuza changamoto tulizokumbana nazo. Ni hakika haukuwa kamilifu lakini tunaamini kwa ujumla tumefanya vizuri sana, japokuwa bado tunayo nafasi ya kuzidi kuuboresha. Na kwa namna yoyote ndiyo maana tuliwaalika waangalizi vikiwemo vyombo vya habari na waangalizi wengine wa uchaguzi, ili kuweza kutangaza habari na tunaweza kujifunza kutokana na ripoti hizi na tunaweza kuendelea kuboresha mchakato wa uchaguzi.", amesema Jega.

Wasimamizi wa uchaguzi wakiwahakikika wapiga kura kabla ya kupiga kura zao.Wachambuzi wa mambo wanasema ushindani ni mkubwa sana kiasi cha kushindwa kutamka mshindi ni nani. Ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa Afrika umesema uchaguzi ulikuwa wa amani lakini wamewataka wananchi wa Nigeria kukubali matokeo.

Uchaguzi nchini Nigeria umefanyika Jumamosi na Jumapili, ambapo wagombea wawili wa kiti cha urais, Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na Muhammud Buhari kutoka chama cha upinzani cha APC na ambaye katika miaka ya nyuma amewahi kuwa kiongozi wa nchini hiyo wakati wa utawala wa kijeshi wanachuana vikali kuwania kiti hicho.
CHANZO:BBC

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA