Posts

Hackers Waigeuza Akaunti ya Instagram ya Fid Q Kuwa ya Wema Sepetu!

Image
Kama unaitafuta akaunti ya Instagram ya Fid Q kuanzia jana bila mafanikio basi fahamu kuwa hackers wameitaifisha, kufuta picha zake zote na kuigeuza kuwa ya Wema Sepetu. Akaunti hiyo ina followers zaidi 160,000. “Account hii imekuwa hacked jana usiku ila mimi nimegundua leo asubuhi,” Fid ameiambia Clouds FM. “ Niligundua baada ya kuingia katika account ikawa inanigomea. Mimi nilikuwa nimeandika mwanaharakati, sasa naona wameamua kubadili na jina na kuandika jina la Wema Sepetu, ” alisema.

THAILAND: “UCHUNGUZI UMEANZISHWA KUJUA ALIYEHUSIKA NA MASHAMBULIZI”

Image
Baadhi ya raia kutoka China, Hong Kong, Malaysia na Singapore ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Bangkok, Jumatatu Agosti 17, 2015. Na RFI Idadi ya watu waliouawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Bangkok, imeongezeka na kufikia 21, huku watu 125 wakiripotiwa kujeruhiwa. baadhi ya raia kutoka China, Hong Kong, Malaysia na Singapore ni miongoni mwa waliouawa. Uraia wa baadhi ya miili iliyopatikana, haujafahamika. Hata hivyo, polisi imemtambua mtuhumiwa mmoja kupitia kamera za usalama ziliowekwa kwenye eneo takatifu kwa watu kutoka jamii ya Hindu ambapo bomu lililipuka. Wizara ya ulinzi ya Thailand inasema kuwa watu waliotega mabomu katika eneo takatifu jijini Bangkong waliwalenga watalii. Wizara hiyo imeongeza kuwa inawasaka waliotega mabomu hayo yaliyolipuka Jumatatu jioni wiki hii na kusabisha vifo vya watu 21 na wengine 120 kujeruhiwa. Eneo hilo lililongwa limekuwa kivutio kikubwa cha watalii na raia wa nchi hiyo amba

OSCAR PISTORIUS KUACHIWA IJUMAA

Image
Mwanariadha Oscar Pistorius. Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wake Reeva Steenkamp. Oscar Pistorius akiwa mahakamani wakati wa kesi yake. Mwanariadha mahiri wa nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius anatarajiwa kuachiwa Ijumaa hii baada ya kuonyesha tabia nzuri akiwa gerezani. Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani mwaka uliopita kwa kosa la kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp katika usiku wa Siku ya Wapendanao 'Valentine's Day'. Pistorius ametumikia kifungo cha miezi 10 pekee gerezani kati ya miaka mitano aliyohukumiwa. Baada ya kuachiwa, Pistorius anatarajiwa kuwa akitumikia muda wake uliobaki akiwa katika kifungo cha nje. Wakati akitoa hukumu ya staa huyo, Jaji Thokozile Masipa alisema kuwa kiongozi wa mashtaka nchini Afrika Kusini alishindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp alipompiga risasi nyumbani kwake akidhani kuwa ni mwizi.

Lulu ‘kajibebisha’ kwa Diamond Platnumz amchokonoa Zari

Image
Chanzo:GPL UCHOKOZI! Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael 'Lulu' anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine baada ya kudaiwa ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz', kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kumchokonoa mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ . Tukio hilo lilijiri usiku mnene Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa House Club uliopo Masaki, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya bethdei ya DJ wa Diamond, Rommy Jones. Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyeweka kambi ukumbini humo, Lulu, bila kujali kwamba, Diamond alimwacha Zari nyumbani akimnyonyesha ‘baby girl’ wao, Latifah Nasibu a.k.a ‘Princess Tiffah’, alionekana akijiachia naye kimahaba huku akionesha ‘kummisi’ kinoma jamaa huyo. ILIANZA HIVI Lulu, alikuwa wa mwishomwisho kuingia ukumbini ambapo baada ya kuzunguka kusalimiana na mastaa wengine alitua kwenye sofa alilokuwa amekaa Diamond ambapo walianza kufanya yao bila kujali ëwavimba machoí wa

TAYARI 3 WAMEFARIKI KWA KIPINDUPINDU DAR, 34 WAMELAZWA

Image
Watu watatu (wanawake 2, mwanaume 1) wamefariki dunia na wengine 34 wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na hospitali ya Mburahati jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kipindupindu. Hospitali ya Sinza Palestina imeripotiwa kuwa na wagonjwa walio na dalili za ugonjwa huo zaidi ya 50. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Paul Makonda amezitaja Kata zilizoathirika na ugonjwa huo kuwa ni Kijitonyama, Kimara, Manzese, Tandale, Saranga, Makumbusho na Mwananyamala. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, amesema kuna ripoti ya wagonjwa waliolazwa 71 hadi sasa, na kwamba Wilaya ya Ilala na Temeke bado hazijakumbwa na ugonjwa huo. Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, Mganga Mkuu wa Minispaa hiyo, Dk. Aziz Msuya, amesema kuwa mgonjwa wa kwanza aligunduliwa katika maeneo ya Kijitonyama kwa Ally Maua na kufia nyumbani kwake katika eneo hilo na kuambukiza ndugu zake wawili ambao walikufa wakati wanapelekwa

SOMA VICHWA VYA MAGAZETI YA LEO JUMATANO, HABARI ZA KITAIFA, MICHEZO NA KIMATAIFA

Image

Meninah aolewa kimyakimya jijini Dar na mtoto wa Waziri

Image
WENYE wivu wajinyonge! Nyota wa muziki wa kizazi kipya, zao la BSS 2012 Meninah Abdulkarim, anadaiwa kufunga ndoa kimyakimya mwishoni mwa wiki iliyopita na mtu anayetajwa kulelewa tangu utotoni na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini aliyejiuzulu, Profesa Sospeter Muhongo. Chanzo chetu makini kimearifu kuwa shughuli hiyo ilifanyika Agosti 16 mwaka huu ikimaliziwa na sherehe kubwa iliyofanywa nyumbani kwao, Kigamboni jijini Dar es Salaam. “Ebwana Meninah kaolewa na jamaa mmoja ambaye tumeambiwa ni mtoto wa Muhongo, ambaye alikuwa naye kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu sasa, ndoa hiyo ilikuwa ya siri maana sisi hatukujua kabisa, ila nilikuwa naenda zangu mjini mara nikakutana na magari ya harusi ndiyo nikajumuika na mimi kula ubwabwa,” kilisema chanzo chetu ambacho kilishuhudia shughuli nzima.   Inadaiwa kuwa bwana harusi amelelewa kwa muda mwingi wa maisha yake na Profesa Muhongo kiasi kwamba watu wa karibu na familia hiyo walifahamu ni mtoto wake wa kumzaa. H