SAUT BORN FIRE..WAS AWESOME!!!!
Serikali ya Wanafunzi ya SAUT jana ilidhihirisha hisia zao za kuwajali wanajamii ya SAUT pale ilipoandaa moja bonge la party lililomshusha mtu mzima ROMA Mkatoliki kwa ajili ya kuwakaribisha Wanafunzi wa mwaka wa kwanza.
Msanii huyo wa Hip Hop nchini Roma Mkatoliki aliwapagawisha wanafunzi wa SAUT kwa kufanya show ya nguvu pande hizo on “Born Fire” ambayo ni event yakuwakaribisha mwaka wa kwanza 2011/2012 inayofanyika mwanzoni mwa kila mwaka wa masomo. Roma jana alipanda majira ya saa sita za usiku na kuanza kwa Akapela iliyowaacha baadhi ya mashabiki wake wapige kelele kwa kuimba Roma!!! Roma !!!Roma!!!..Roma alimaliza na kibao chake cha Mathematics kilichowaacha mashabiki hoi katika tukio hilo.
Pata matukio yote katika picha…..

Hata Kwetu wapo ..the local Artist in Mwanza akisababisha mbele ya mashabiki huku Msema Chochote Anatory akiwa nyuma yake (mwenye red)..

Wadau wa PR nao walikuwepo pande izo...Kulia ni John Kalipso na ndugu yake Von Don Kisasa a.k.a Unyayo au CEO wa PR SAUT..

Katikati ni Mdau Asha akiwa na Roda kulia pamoja na friend yao..nao walikuwepo pande zile wakishow love..

Twende kushoto shoto sho, rudi kulia lia li, cheza kizulu zulu zu...ilikuwa full shangwe aiseee arifu...

Haikuwa wanachuo pekee hata wananchi wengine jijini Mwanza walipata time kuparty pamoja,...iyo style hapo kichwani sijui ndo inaitwaje..maana !!!!

George hapo nyuma unamuonea wivu Unyayo au..!! Haya Bi Joy hapo kushoto nawe mbona umemkumbatia sana Bw. Unyayo..Mbogo Junior hapo kushoto niaje naona una Kili Time moja Baridiii!!!!

Mwisho wa siku Nimelewa tilalilaaaaaaa...jamaa alizima hapa aisee..anapatiwa huduma ya kwanza...kumbe sio chai ee..
PICHA NA HABARI NI KUTOKA www.tzcampusvibe.wordpress.com kutoka kwa mdau Mrope Hassan.
Comments
Post a Comment