SEMINA YA SSPRA YAFANA SIKU YA JUMAMOSI


Wanachama wa SSPRA wakisikiliza kwa makini wakati wa semina
kutoka kushoto ni Jacqueline Patrick(Katibu msaidizi),Christopher Ngonyani (Katibu), Wilfried Medard (Makamu mwenyekiti) wakiwa katika semina ya kuijenga SSPRA
Jacqueline Patrick(Katibu msaidizi)

Wilfried Medard (Makamu mwenyekiti)


Albert Tibaijuka (Patron)akitoa busara zake kwa wanachama wa SSPRA
Ndugu Msafiri Lawrence ambaye ni mhitimu wa Shahada ya Uhusiano wa Umma na Masoko akitoa husia kwa wanachama wa SSPRA

Albert Tibaijuka (Patron)

wanachama na viongozi wa SAUT STUDENTS PUBLIC RELATIONS ASSOCIATION (SSPRA) jumamosi ya mwisho wa wiki hii walifanya semina ya kuwakaribisha mwaka wa kwanza na pia kuwakumbusha wanachama wa zamani juu ya kazi na majukumu ya SSPRA katika hali ya kukijenga na kukiimarisha chama hicho semina iliyofanyika katika moja ya madarasa chuoni hapo ndani ya jengo la Mwanjonde.

Aidha akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Kikao hicho ndugu Frank Mashauri alianza kwa kumkaribisha Makamu mwenyekiti wa SSPRA ndugu Wilfred Medard, Bw. Wilfred alianza kwa utambulisho wa Viongozi wa chama hicho pamoja na wajumbe kutoka kamati mbalimbali za chama hicho, ambapo baadae aliweza kutoa malengo na madhumuni ya chama hicho ili kutoa mwanga kwa wanachama wapya kufahamu nini majukumu ya chama hicho.

Akizungumza katika semina hiyo Mlezi wa SSPRA Bw. Albert Tibaijuka ambae pia ni mwalimu wa fani hiyo alielezea historia fupi ya Chama hicho ambapo ilianza kwa Wanafunzi wa Mass Communication waliokuwa wanasoma Public Relations mwaka 2007, Mr. Tibaijuka aliwaeleza wanachama wa chama hicho juu ya upendo, kuheshimiana pamoja na kuwajibika katika kuijenga SSPRA. Akidokeza madhumuni ya Ofisi ya Public Relations kwa mwaka huu Bw. Tibaijuka alisema kuwa Department ya Public Relations ipo katika mchakato wa kuomba Public Relations Laboratory kwa uongozi wa chuo ambayo itatumika na wanafunzi wa Public Relations kufanya shughuli zao za kimasomo, pia department ipo katika mchakato wa kutengeneza kamati ya mahafali ya mwaka huu ikilenga kuandaa sherehe ya pamoja kwa kuangalia miaka 50 ya uhuru na muelekeo mzima wa Public Relations nchini.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA