Posts

Showing posts from August, 2012

Ijumaa hii usikose Uzinduzi wa Santuri 5 kwa pamoja ndani ya NEW MSASANI CLUB

Image

FACES ZA MISS MWANZA HIZI HAPA!! SHINDANO KUFANYIKA IJUMAA HII, NDANI YA YATCH CLUB MWANZA!!

Image

: MAHAKAMA KUU YAMVUA UBUNGE DR DALAL KAFUMU WA CCM

Image
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora imetengua matokeo ya Ubunge wa Mbunge wa jimbo la Igunga Mh. Dalaly Peter Kafumu ambaye alichukua nafasi hiyo baada ya mbunge wa zamani wa jimbo hilo Rostam Azizi Kujiuzulu. Mahakama hiyo imemvua Ubunge Dk. Kafumu hii leo katika Hukumu ya kesi ya Kupinga matokero iliyofunguliwa na aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Chadema, Joseph Kashindye dhidi ya Dk Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi.   Mbali na Dk Kafumu, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi huo, Protace Magayane. Shauri hilo lilianza kusikilizwa rasmi Machi 26 na Jaji Mary Shangal i. Zaidi ya malalamiko 13 yaliwasilishwa katika Mahakama hiyo.

MWENGE WA UHURU WAINGIA MKOANI MARA UKITOKEA MKOANI ARUSHA

Image
                                       Mbio za Mwenge wa uhuru zaanza mkoani Mara       Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw, Clement Lujaji akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru                  Mkuu wa wilatya ya Butiama Bi Angelina Mabula akiwa ameushika Mwenge wa uhuru                     Mkuu  wa wilaya ya Musoma Bw Jackson Msome akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru                        Burudani ni sehemu za mbio hizo za Mwenge   Chanzo: www.mwanawaafrika.blogspo...

WANAHABARI MARA WAPIGWA MSASA KUANDIKA HABARI ZA AFYA

Shomari Binda MUSOMA MUUNGANO wa vilabu vya waandishi wa habari nchini UTPC, umenza kutoa mafunzo maalum kuandika habari za afya kwa waandishi wa habari katika mikoa yote nchini. Hatua hiyo inalenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari za afya zilizofanyiwa utafiti wa kina kwa lengo la kuboresha sekta afya na kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii. Mkurugenzi wa UTPC Bw Aboubakar karssan, ameyasema hayo mjini Musoma wakati wa mafunzo ya kwanza ya siku nne kuanza kutolewa nchini kwa waandishi wa habari mkoani Mara ikiwa ni sehemu ya utatuzi wa matatizo na kuibua changamoto zinazokabili utoaji wa huduma ya afya nchini. Amesema kwa muda mrefu jamii imekuwa ikikabiliwa na sintofahamu juu ya kujikinga na maambukizi ya magonjwa hususan Ukimwi kutokana na waandishi nchini kutoandika habari ambazo zimefanyiwa utafiti wa kina ambao haotoi majibu ya namna ya kujikinga na maambukizi mapya. Kwa sababu hiyo ametoa wito kwa wanahabari mkoani Mara kutumia vem...

HII VIDEO NAIKUBALI SANA Pah One - Ghetto (aika,igwee,ola,nahreel)

HII VIDEO KIUKWELI KATIKA MAZINGIRA AMBAPO IMETENGENEZEWA INAWEZA KUKUSTAJABISHA LAKINI NDIO MAZINGIRA HALISI,SEHEMU AMBAYO KUNA UCHAFU WA KUTOSHA LAKINI ADAM JUMA KAFANYA KWELI.

DJ Choka ft. Leo,Mabeste,Baghdad,Cyrill,Shetta,Noorah,Young D,Stereo,Deddy - PAMOJA WE CAN

Image

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 12/08/2012!

Image
. . . . . . . . . . . .

TAKUKURU YAMFIKISHA ALIYEKUWA MHANDISI BUNDA MAHAKAMANI

Na Shomari Binda Musoma, Taasisi ya kuzui na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Mara imemfikisha Mahakamani Christopher Nyandiga aliyekuwa Mhandisi wa Halimashauri ya Wilaya ya Bunda ambaye kwa sasa amehamishiwa Wilaya ya Ludewa kwa makosa ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajili kinyume cha kifungu cha 22 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007. Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari,Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mara Yustina Chagaka ilisema kutokana na uganganyifu huo ameisababishia Serikali hasara ya jumla ya shilingi za Kitanzania milioni ishirini na nne (24,000,000) kinyume cha kifungu cha 10(1) cha jedwali la kwanza pamoja na vifungu vya 57(1) na 60(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi namba 200 iliyofanyiwa mapitio Mwaka 2002. Alisema baada ya Uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU ulibaini kampuni inayomilikiwa na mtuhumiwa huyo iitwayo MBULLY ENTERPRISES AND CIVIL WORK ilipewa zabuni na Halimashauri na Wilaya ya ...

Ushauri wa Ziro kuhusu medali za Ulimbiki (Olimpiki)

Image
 

CHEKI KICHUPA KIPYA CHA MALFRED- My Desire

Image

TUSIWAUMIZE WENZETU KWA KUWAVISHA PETE ZA UCHUMBA

Siku mbili zilizopita nilipata message kutoka kwa rafiki yangu ambaye  ni msichana...kiukweli nilipatwa na kigugumizi cha mikono ni kwa jinsi gani nitaweza kumshauri kwa kupitia ujumbe mfupi wa mkononi yaani sms aweze kuona kwamba swala lililomtokea ni la kawaida kwa maana kwamba binadamu tumeumbiwa matatizo na ni jukumu letu kupambana nayo mpaka kupata suluhisho la matatizo hayo. Story ilikuwa hivi,dada huyu ambaye ndio rafiki yangu alinitumia message akiniambia kuwa miezi 2 iliyopita amevalishwa pete ya ndoa na mchumba wake, sasa cha kushangaza ni kwamba wamekuwa katika mahusiano na mchumba wake huyo kwa muda wa miaka 2 bila binti kujua lolote kuwa mchumba wake alishazaa na mwanamke mwingine japokuwa  binti alisha muuliza mchumba wake huyo kama ana mtoto lakini jamaa alikuwa akipinga vikali kuwa hajawai na wala hana hata wa kusingiziwa, jibu ambalo lilikuwa lkimfurahisha dada huyu na pia kuambiwa kuwa yuko peke yake  hana mahusiano mengine ya nje. Utamu w...

GHARAMA ZA MATIBABU VYUONI NI MRADI WA VYUO HUSIKA?

MAKALA HII IMEANDALIWA NA  ANTHONIUS CLEMENT Mwanafunzi wa chuo kikuu cha mt.Augustino anayesomea shahada ya mahusiano ya Umma na Masoko mwaka wa pili. Email: tonyboy1989@yahoo.com Mobile: + 255 717437729 /+255762 963674 Wengi wetu tunafahamu   juu ya umuhimu wa Afya katika jamii yoyote ile. Jamii yenye Afya bora ndiyo yenye maendeleo makubwa kijamii na hata kiuchumi. Nakatika   suala hili siwezi kusita kumzungumzia mwanazuoni   anayea julikana   kama Vans Parkard mwanazuoni huyu wa saikolojia na masomo ya sayansi ya jamii na hasa mawasiliano aliweza kuanisha mahitaji makuu nane ya mwanadamu, Moja ya hitaji hilo ni hitaji la kuishi muda murefu (Imotarity needs) .   Hitaji hili ndilo linalo wafanya watu wahangaike kwa muda mrefu waki jipodoa ilimradi tu waonekane bado vijana wabichi. Mwaka mmoja nanusu uliopita Watanzania tuliweza kushuhudia wananchi wengi wakifurika katika kitongoji cha Semunge huko Loliondo alimaarufu “ kwenye kikombe...

TANZANIA MUSIC FESTIVAL COMMING SOON

Image

ATHARI ZA KUJITOA KATIKA FAO LA UZEENI

Makala hii imejumuisha mawazo ya wale wote waliochangia kwenye hoja ya haja juu ya dhana ya mifuko ya hifadhi ya jamii, niliyoiweka kwenye blog hii tarehe 31.07.2012. Asante kwa mawazo ya kujenga na kwa paomoja tuijenge Tanzania yetu. Natumaini tunaweza kukubaliana kuwa sera yoyote hupimwa ufanisi wake kwa kuzingatia inatekelezwaje mkabala na mahitaji ya uanzishwaji wake.Hakuna sera isiyokuwa na lengo, lengo likitimia ndipo tunapoweza kubaini   kuwa sera imefaulu au imeshindwa. Dhana na lengo la mifuko ya hifadhi ya jamii ni kuwakinga wananchi ( wafanyakazi wa umma, binafsi, walioajiliwa na waliojiajili ) dhidi ya matukio yasiyo tarajiwa   maana ambayo ni bayana. Lakini tukumbuke kuwa, neno “ jamii ” katika sera hii linatuvuta kuangaliazaidi ya mteja wa mifuko ya hifadhi ya jamii, lakini pia watu na taasisi zinazowazunguka ambazo   kwa njia moja au nyingine huweza kuathiriwa na matendo ya mteja   wa mifuko ya hifadhi ya jamii, hii ndio maana mifuko mingi ya hi...