TAKUKURU YAMFIKISHA ALIYEKUWA MHANDISI BUNDA MAHAKAMANI
- Get link
- X
- Other Apps
Na Shomari Binda
Musoma,
Taasisi ya kuzui na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Mara
imemfikisha Mahakamani Christopher Nyandiga aliyekuwa Mhandisi wa
Halimashauri ya Wilaya ya Bunda ambaye kwa sasa amehamishiwa Wilaya ya
Ludewa kwa makosa ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajili
kinyume cha kifungu cha 22 cha Sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa
namba 11 ya mwaka 2007.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya
Habari,Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mara Yustina Chagaka ilisema
kutokana na uganganyifu huo ameisababishia Serikali hasara ya jumla ya
shilingi za Kitanzania milioni ishirini na nne (24,000,000) kinyume cha
kifungu cha 10(1) cha jedwali la kwanza pamoja na vifungu vya 57(1) na
60(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi namba 200 iliyofanyiwa mapitio Mwaka
2002.
Alisema baada ya Uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU
ulibaini kampuni inayomilikiwa na mtuhumiwa huyo iitwayo MBULLY
ENTERPRISES AND CIVIL WORK ilipewa zabuni na Halimashauri na Wilaya ya
Bunda ya kuleta mashine ya windmill aina ya Poldaw ya mita 5.8 na mita
8.2 kwa gaharama ya shilingi milioni ishirini na nne kwa ajili ya mradi
wa umwagiliaji mazao katika kijiji cha Kasuguti na kuleta vilivyo
chakavu na visivyofaa kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Taarifa hiyo
iliieleza kuwa mtuhumiwa huyo pia aliwasilisha gharama ya shilingi
milioni mbili(2,000,000) kwa ajili ya kuisimika na shilingi milioni
(1,000,000,) yakuifanyia majaribio mashine hizo na kufanya jumla ya
shilingi milioni ishirini na saba (27,000,000) kwa ajilki ya mradi huo.
Ushunguzi huo wa TAKUKURU ulibini mnamo Desemba 2007 mtuhumiwa huyo kwa
niaba ya kampuni ya MBULLY ENTERPRISES AND CIVIL WEORKS aliwasilisha
hati ya madai (invoice) nambari 0152 na (delivery Note) nambari 0252 kwa
Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Bunda zenye maelezo ya uongo
kwamba amenunua mashine mpya huku zikiwa ni chakavu na zisizofaa na
kuisababishia Serikali hasara.
Kufuatia hali hiyo,Mkuu wa
TAKUKURU Mkoa wa Mara Chagaka alitoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa
ushirikiano kwa kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa wanapoona mazingira
ya kufanyika.
Alisema kazi ya kupambana na vitendo vya Rushwa
katika sehemu mbalimbali haifanywi na Taasisi hiyo pekee yake bali kila
Mwananchi anapaswa kushiriki ili kuweza kukomesha vitendo hivyo kwa kuwa
vinafifisha shughuli za kimaendeleo na kutopatikana huduma iliyo
sahihi.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari,Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mara Yustina Chagaka ilisema kutokana na uganganyifu huo ameisababishia Serikali hasara ya jumla ya shilingi za Kitanzania milioni ishirini na nne (24,000,000) kinyume cha kifungu cha 10(1) cha jedwali la kwanza pamoja na vifungu vya 57(1) na 60(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi namba 200 iliyofanyiwa mapitio Mwaka 2002.
Alisema baada ya Uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU ulibaini kampuni inayomilikiwa na mtuhumiwa huyo iitwayo MBULLY ENTERPRISES AND CIVIL WORK ilipewa zabuni na Halimashauri na Wilaya ya Bunda ya kuleta mashine ya windmill aina ya Poldaw ya mita 5.8 na mita 8.2 kwa gaharama ya shilingi milioni ishirini na nne kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji mazao katika kijiji cha Kasuguti na kuleta vilivyo chakavu na visivyofaa kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Taarifa hiyo iliieleza kuwa mtuhumiwa huyo pia aliwasilisha gharama ya shilingi milioni mbili(2,000,000) kwa ajili ya kuisimika na shilingi milioni (1,000,000,) yakuifanyia majaribio mashine hizo na kufanya jumla ya shilingi milioni ishirini na saba (27,000,000) kwa ajilki ya mradi huo.
Ushunguzi huo wa TAKUKURU ulibini mnamo Desemba 2007 mtuhumiwa huyo kwa niaba ya kampuni ya MBULLY ENTERPRISES AND CIVIL WEORKS aliwasilisha hati ya madai (invoice) nambari 0152 na (delivery Note) nambari 0252 kwa Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Bunda zenye maelezo ya uongo kwamba amenunua mashine mpya huku zikiwa ni chakavu na zisizofaa na kuisababishia Serikali hasara.
Kufuatia hali hiyo,Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mara Chagaka alitoa wito kwa Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa wanapoona mazingira ya kufanyika.
Alisema kazi ya kupambana na vitendo vya Rushwa katika sehemu mbalimbali haifanywi na Taasisi hiyo pekee yake bali kila Mwananchi anapaswa kushiriki ili kuweza kukomesha vitendo hivyo kwa kuwa vinafifisha shughuli za kimaendeleo na kutopatikana huduma iliyo sahihi.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment