GHARAMA ZA MATIBABU VYUONI NI MRADI WA VYUO HUSIKA?
MAKALA HII IMEANDALIWA NA
ANTHONIUS CLEMENT
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha mt.Augustino anayesomea shahada ya mahusiano ya Umma na Masoko mwaka wa pili.
Email:tonyboy1989@yahoo.com
Mobile: + 255 717437729 /+255762 963674
Wengi wetu
tunafahamu juu ya umuhimu wa Afya katika
jamii yoyote ile. Jamii yenye Afya bora ndiyo yenye maendeleo makubwa kijamii
na hata kiuchumi. Nakatika suala hili
siwezi kusita kumzungumzia mwanazuoni anayea
julikana kama Vans Parkard mwanazuoni
huyu wa saikolojia na masomo ya sayansi ya jamii na hasa mawasiliano aliweza
kuanisha mahitaji makuu nane ya mwanadamu, Moja ya hitaji hilo ni hitaji la
kuishi muda murefu (Imotarity needs).
Hitaji hili
ndilo linalo wafanya watu wahangaike kwa muda mrefu waki jipodoa ilimradi tu
waonekane bado vijana wabichi. Mwaka mmoja nanusu uliopita Watanzania tuliweza
kushuhudia wananchi wengi wakifurika katika kitongoji cha Semunge huko Loliondo
alimaarufu “ kwenye kikombe cha babu”hii inadhirisha umuhimu wa kuwa na Afya na siha njema kwa ujumla.
Hapa nchini
Tanzania dhamana ya afya
imewekwa chini ya taasisi muhimu inayo shughulikia huduma za afya kwa
kuwasaidia wamanchi wote kupata huduma za Afya kwa gharama nafuu kabisa.Taasisi
hii inajulikana kama Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya .
Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya ulianzishwa mahususi chini ya sheria ya ya bunge namba 8
ya mwaka 1999 sura namba 395 toleo la mwaka 2002.Bima ya Afya ilianzishwa
mahususi kwaajiri ya kukidhi hitaji la
usalama wa Afya kwa watanzania wote nakwa kuanza ilianza kuwa hudumia watu
waliopo katika sekta rasmi za kazi na
kufuatia mabadiliko ya sheria hivi sasa Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya unahusisha hata watu wasio katika sekta rasimi
kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
Kwakuona
kuna baadhi ya ya makundi yameachwa na
na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ulianzishwa utaratibu wa kutoa matibabu kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Utaratibu huu unalenga kuwapa Bima ya Afya wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu popote nchini ambapo humwezesha mwanafunzi kupata huduma za matibabu wakati wote awapo masomoni
nawakati wa likizo katika muhula husika.
Chini ya
utaratibu wa Mfuko wa Taifa wa bima ya
Afya chuo husika huwaandikisha wanafunzi wake kama mdhamini wa wanfunzi hao,pia kunamkataba wa maridhiano
baina na Mfuko waTaifa wa bima ya Afya ,vilevile mkataba
baina ya mwanafunzi na na bima ya afya
(NHIF)niwa kipindi cha miaka mitatu na hurejewa kila mwaka .pia baada ya mwanafunzi kuhitimu chuo huwa na jukumu la
kurudisha kadi ya uanachama kwani mkataba na mwanfunzi husika huwa umekwisha.
Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) pamoja na kuingia mkataba kati ya chuo na
mwanafunzi umetoa mchanganuo juu ya namna gani michango ina wasilishwa,mchanganuo
huo ni kama ifuatavyo: Mwanafunzi
hulazimika kuchangia shilingi za kitanzania 4,200 kwa mwezi sawa na shilingi
50,400 kwa mwaka!mwanafunzi akisha changia
mchango atapata matibabu kwa kipindi chote cha mwaka wa masomo pia hata
awapo likizo. Ifahamike hapa kuwa kuna
baadhi ya wanafunzi wana bima za Afya hivyo utara tibu huu wao hauwahusu kwani
wao tayari ni wanchama na wana vitambulisho vyao na wanapata huduma za matibabu
kama kawaida.
Baadhi ya
vyuo hapa nchini vimeshindwa kuridhia makubaliano ya mkataba kati yake na mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya, hapa Hapa maswali mengi yanaweza kuzuka labda ni mradi
wa vyuo husika? ni kwanini vyuo hivi vinashindwa kuridhia makubaliano na mfuko
huu wenye lengo la kutoa huduma za kiafya kwa Watanzania wote nchini na kwa
gharama nafuu.
Kwa mfano chuo
cha Mtakatifu Agustino kinao utaratibu wa
kila mwanafunzi kulipia shilingi 100,000 kila mwaka kwaajiri ya matibabu pindi
awapo masomoni lakini bado huduma zinazo tolewa ni duni na hazikizi mahitaji,vilevile
mwanfunzi pindi auguapo wakati wa likizo hulazimika kujigharimia yeye
mwenyewe gharama za matibabu!!
Ukiondoa chuo
Kikuu cha Dodoma ambacho wanafunzi hulipia shilingi 100,00 nakupewa huduma za
matibabu kwa miaka yote mitatu,Pia chuo
cha CBE navingine vingi vina utaratibu kama huo ambapo mwanafunzi hulazimika
kulipa zaidi ya shilingi 90,000 kila
mwaka kwaajiri ya matibabu.Kwa mifano hii tunaweza kuona ni jinsi gani
wanafunzi wa baadhi ya vyuo vikuu hapa nchini wanakumbana na adha ya matibabu
pindi wauguapo aidha wakiwa masomon, pia wakati wa likizo hulazimika kuji gharimia wenyewe
matibabu.
Ukilinganisha
na vyuo hapa nchini kama,Chuo Kikuu cha Dar-es salaam,SUA,pamoja na Mzumbe vyuo
hivi tayari vimekwisha ridhia mkataba na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Wanafunzi
wa vyuo hivi hupata matibabu pindi wawapo masomoni nahata wakati wa likizo kwa
gharama ya shilingi 50,400 tu kwa mwaka mzima.
Binafsi
najiuliza kwanini baadhi ya vyuo havijaridhia
kuingia mkataba na Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya ili kuwapunguzia gharama za matibabu wanafunzi hawa ambao wengi
wao wanatoka katika familia zenye kipato cha chini au kwa jina maarufu “Watanzania wa kawaida”.
Panadol ya
pasua kichwa hii juu ya suala la huduma za Afya ni kwa uongozi wa vyuo husika
pamoja na uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kushilikiana kwa
pamoja ili kuwasaidia wanafunzi hawa dhidi ya gharama za matibabu zinazoendela
kupanda kila siku uchao na uchwao!!
Comments
Post a Comment